Pata taarifa kuu
ZIMBABWE

Umoja wa Afrika wakaribisha kujiuzulu kwa Robert Mugabe

Umoja wa Afrika umekaribisha uamuzi wa Robert Mugabe kujiuzulu kama rais wa Zimbabwe.

Mkuu wa Tume ya Umoja wa Afrika Moussa Faki Mahamat.
Mkuu wa Tume ya Umoja wa Afrika Moussa Faki Mahamat. Flickr/CC/Chatham House/©Suzanne Plunkett 2017
Matangazo ya kibiashara

Mkuu wa Tume hiyo Moussa Faki Mahamat amesema wananchi wa Zimbabwe wamesikika kwa kutaka mabadiliko ya amani.

Aidha, amesema kuwa Mugabe atakumbukwa kwama mtu aliyesimamia Umoja wa Afrika na baba wa uhuru wa taifa lake la Zimbabwe.

Licha ya jeshi kuingilia siasa za Zimbawe Umoja wa Afrika, haukusema hatua hiyo kuwa mapinduzi ya kijeshi na kukemea.

Umoja wa Afrika huwa hautambui mabadiliko ya serikali kupitia mapinduzi ya kijeshi kama ambayo ilivyokuwa inafanyika katika mataifa mengi miaka iliyopita.

'Umoja wa Afrika, unatambua kuwa wananchi wa Zimbabwe wamezungumza na kuhakikisha kuwa, demokrasia inadumu katika nchi yao,” amesema Mahamat.

 

 

 

 

 

 

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.