Pata taarifa kuu
NIGERIA-BOKO HARAM

Watu 50 wapoteza maisha katika shambulizi la kigaidi nchini Nigeria

Takribani watu 50 wamepoteza maisha kufuatia shambulio la bomu la kujitoa muhanga lilitokea katika msikiti mmoja kaskazini mashariki mwa Nigeria. Kundi la Boko Haram linadaiwa kuhusika.

Eneo la shambulio la awali la mshambuliaji wa kujitoa muhanga nchini Nigeria.
Eneo la shambulio la awali la mshambuliaji wa kujitoa muhanga nchini Nigeria. REUTERS/Afolabi Sotunde
Matangazo ya kibiashara

Shambulizi hili la kujitoa mhanga, limetokea katika mji wa Mubi katika jimbo la Adamawa, kwa mujibu wa ripoti za polisi.

Msemaji wa Polisi katika mji huo Othman Abubakar, amethibitisha shambulizi ndani ya msikiti huo na kulishtumu kundi la kigaidi la Boko Haram kuhusika.

Ahmad Al Hassan wa Idhaa ya RFI Hausa amezungumza na Musa Hamad Belo, Mwenyekiti wa Manispaa wa mji wa Mubi, ambaye alimueleza kuwa shambulio hilo linatisha.

Hili ni shambulizi baya zaidi kuwahi kutekelezwa nchini humo na kusababisha idadi kubwa ya watu kwa wakati mmoja.

Taarifa zinasema kuwa mshambuliaji aliingia katika msikiti huo na kuungana na waumini katika ibada ya asubuhi na kutekeleza shambulio hilo.

Othman Abubakar ameeleza kuwa raia wengi wamejeruhiwa ingawa hakutaja idadi kamili huku akikiri kuwa kuwa majeruhi wote wamepelekwa hospitali kwa matibabu zaidi.

Abubakar ameeleza hakuna ushahidi wa moja kwa moja kuhusu anayehusika na shambulio hilo ingawa amekiri kuwatambua wote wlio nyuma ya matukio kama hayo.

Imeripotiwa kundi la wapiganaji la boko Haramu limekuwa likitekeleza mashambulio yaliyosababisha vifo vya takribani raia elfu 20 na wengine zaidi ya million 2 wakikosa makazi tangu mwaka 2009.

Linasalia kundi hatari sana kwa usalama wa nchi hiyo na nchi jirani, huku juhudi za serikali zikiwa bado hazijazaa matunda.

Nigeria, imeugana na mataifa mengine kama Cameroon, Niger, Benin na Chad katika makabiliano ya kundi hili hatari.

Magaidi hao wanaokadiriwa kuwa kati ya 15,000 hadi 20,000 wanaaminika kujificha katika msitu wa Sambisa Kaskazini mwa nchi hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.