Pata taarifa kuu
ZIMBABWE-SIASA-USALAMA

Chama cha Zanu-PF chamtaka Robert Mugabe kuachia ngazi mara moja

Chama tawala nchini Zimbabwe, Zanu-PF, kimetangaza Jumapili hii (Novemba 19) kuwa kitaandaa utaratibu wa kumtimua Rais Robert Mugabe bungeni kuachia ngazi kabla ya kesho Jumatatu Novemba 20.

Robert Mugabe, mwenye umri wa miaka 93, afukuzwa kwenye uongozi wa chama cha wa Zanu-PF, Mkewe Grace Mugabe afukuzwa katika chama cha Zanu-PF.
Robert Mugabe, mwenye umri wa miaka 93, afukuzwa kwenye uongozi wa chama cha wa Zanu-PF, Mkewe Grace Mugabe afukuzwa katika chama cha Zanu-PF. REUTERS/Philimon Bulawayo
Matangazo ya kibiashara

Kwa upande mwingne, chama cha Zanu-PF kimemteua Emmerson Mnangagwa kupeperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi wa mwaka 2018.

"Ndugu yetu Robert Mugabe lazima ajiuzulu kwenye wadhifa wa uongozi wa Zimbabwe kama hakufanya hivyo kabla ya siku ya Jumatatu mchana (...) Spika wa Bunge" ataanzisha utaratibu wa kumng'atua mamlakani, msemaji wa Zanu-PF Simon Khaye Moyo amesema katika mkutano wa dharura wa chama hicho. Mapema leo asubuhi, Rais Mugabe alifukuzwa kutoka nafasi yake ya uongozi wa chama cha Zanu-PF.

Wakati huo huo Emmerson Nangagwa, Makamu wa rais, aliyefutwa kazi hivi karibuni, ameteuliwa kuchukua nafasi ya Robert Mugabe kama kiongozi wa chama cha Zanu-PF. Pia ameteuliwa kupeperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi wa urais wa mwaka 2018.

Maelfu ya watu nchini Zimbabwe waliingia barabarani siku ya Ijumaa kuandamana kumpinga Bw. Mugabe.

Bw. Mugabe anatarajiwa kukutana na makanda wa jeshi na msafara wa magari umeonekana ukiondoka makao ya rais.

Mkuu wa chama chenye nguvu cha wale waliopigania uhuru Chris Mutsvangwa, aliiambia Reuters kuwa chama kilikuwa kinaanza mchakato wa kumuondoa Mugabe madarakani kama rais.

Grace Mugabe afukuzwa katika chama

Leo asubuhi vugu vugu la vijana kutoka chama tawala cha Zanu-PF pia lilichukua uamuzi wa kumfukuza mkewe Robert Mugabe, Grace Mugabe katika vugu vugu hilo. Saa chache baadaye mkutano wa dharura wa chama  cha Zanu-PF ulichukua uamuzi kumfukuza katika chama cha hicho.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.