Pata taarifa kuu
ZIMBABWE-SIASA-USALAMA

Mugabe afutilia mbali wito wa kumtaka ajiuzulu

Baada ya mkutano kati ya ujumbe wa Afrika kusini wawakilishi wa jeshi na Rais Robert Mugabe katika ikulu mjini Harare siku ya Alhamisi, Rais Mugabe anaripotiwa kukataa kuachia ngazi licha ya kuongezeka wito wa kumtaka ajiuzulu.

Robert Mugabe na Mkuu wa majeshi ya Zimbabwe, Jenerali Chiwenga katika ikulu mjini Harare, Novemba 16, 2017.
Robert Mugabe na Mkuu wa majeshi ya Zimbabwe, Jenerali Chiwenga katika ikulu mjini Harare, Novemba 16, 2017. ZIMPAPERS/Joseph Nyadzayo/Handout via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa ulinzi wa Afrika Kusini na Waziri wa Usalama wa Taifa, waliotumwa nchini Zimbabwe na Rais Jacob Zuma, ambaye kwa sasa ni rais wa Jumuiya ya nchi za kanda ya kusini mwa Afrika (SADC), walkutana na Robert Mugabe ikulu mjini Harare.

Lakini hakuna taarifa rasmi iliyotolewa kuhusu mazungumzo yaliyofanywa na Muganbe na ujumbe kutoka Afrika Kusini.

Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe anaamini kuwa bado yuko kiongozi halali wa Zimbabwe na kupinga shinikizo kutoka kwa jeshi linalotaka kumuondoa mamlakani, vyanzo vya siasa na vile vilivyo karibu na idara ya ujasusi vimebaini.

Hata hivyo mpinzani wake wa muda mrefu Morgan Tsvangirai amemtaka ajiuzulu mara moja kwa maslahi ya taifa.

Makamu wa zamani wa Rais Mugabe, Joice Mujuru, pia ametaka kuwe na serikali ya mpito na pia uchaguzi huru na wa kuaminika.

Siku moja baada ya jeshi kuchukua udhibiti wa Zimbabwe, chanzo cha kisiasa kinasema rais Mugabe hana nia ya kujiuzulu kabla ya uchaguzi uliopangwa kufanyika mwaka ujao.

Wachanganuzi wa siasa za kimataifa wanasema kuwa Rais Mugabe anaweza kujaribu kujihakikishia usalama na familia yake kabla ya kuondoka madarakani.

Kasisi kutoka kanisa Katoliki, Fidelis Mukonori anajaribu kusuluhisha pande mbili husika katika mvutano huo, ikiwa ni pamoja na rais Mugabe na jeshi, ambalo lilichukua udhibiti wa nchi usiku wa Jumanne kuamkia Jumatano, likibaini kwamba linawasaka wahalifu walio karibu na Rais Mugabe, mwenye umri wa miaka 93 ambaye yuko madarakani kwa miaka 37.

Majadiliano yanalenga kuunda serikali ya mpito kwa utulivu bila damu kumwagika.

Waziri wa zamani wa Fedha Tendai Biti amesema yuko tayari kujiunga na serikali ya umoja wa kitaifa ikiwa Morgan Tsvangirai atashiriki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.