Pata taarifa kuu
ZIMBABWE-SIASA-USALAMA

Robert Mugabe aendelea kukabiliana na shinikizo la jeshi

Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe anaamini kuwa bado yuko kiongozi halali wa Zimbabwe na kupinga shinikizo kutoka kwa jeshi linalotaka kumuondoa mamlakani, vyanzo vya siasa na vile vilivyo karibu na idara ya ujasusi vimebaini.

Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe adai kuwa bado ni kiongozi halali wa Zimbabwe
Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe adai kuwa bado ni kiongozi halali wa Zimbabwe REUTERS/Philimon Bulawayo
Matangazo ya kibiashara

Siku moja baada ya jeshi kuchukua udhibiti wa Zimbabwe, chanzo cha kisiasa akinasema rais Mugabe hana nia ya kujiuzulu kabla ya uchaguzi uliopangwa kufanyika mwaka ujao.

"Ni aina fulani ya mvutano, ni hali tete," kimesema chanzo hicho, ambacho kiliweza kuzungumza na ndugu wa rais Mugabe, ambaye yeye na familia yake wako chini ya kifungo cha nyumbani katika ikulu ya rais mjini Harare.

"Wanasema rais anapaswa kumaliza muhula wake."

Kasisi kutoka kanisa Katoliki, Fidelis Mukonori anajaribu kusuluhisha pande mbili husika katika mvutano huo, ikiwa ni pamoja na rais Mugabe na jeshi, ambalo lilichukua udhibiti wa nchi usiku wa Jumanne kuamkia Jumatano, likibaini kwamba linawasaka wahalifu walio karibu na Rais Mugabe, mwenye umri wa miaka 93 ambaye yuko madarakani kwa miaka 37.

Majadiliano yanalenga kuunda serikali ya mpito kwa utulivu bila damu kumwagika.

Waziri wa zamani wa Fedha Tendai Biti amesema yuko tayari kujiunga na serikali ya umoja wa kitaifa ikiwa Morgan Tsvangirai atashiriki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.