rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Equatorial Guinea Teodoro Obiang Ufaransa

Imechapishwa • Imehaririwa

Mahakama nchini Ufaransa yampa kifungo cha nje Makamu wa rais wa Equatorial Guinea

media
Makamu wa rais wa Equitorial Guinea Teodorin Nguema Obiang AFP

Mahakama jijini Paris Ufaransa imemhukumu kifungo cha nje cha miaka mitatu jela Makamu wa rais Teodorin Obiang, mtoto wa rais wa Equitorial Guinea Teodore Obiang Nguema baada ya kumpata na kosa la kuiba fedha za umma.


Kesi dhidi ya Makamu huyo wa urais mwenye umri wa miaka 48 iimeendesha na ofisi mbili za waendesha mashataka wa Ufaransa wamemtuhumu kwa kuishi maisha ya kifahari Jijini Paris ikiwa kesi ya kwanza ya kigogo wa juu kutoka familia za viongozi barani Afrika.

Wakati hukumu hiyo ikitolewa, Teodorin hakuwepo Mahakamani na majaji waliotoa hukumu wameamuru pia kulipa Dola za Marekani Milioni 35 kutokana na ubadhirifu, utakatishaji wa fedha na matumizi mabaya ya madaraka.

Katika kipindi cha wiki tatu za usikilizwaji wa kesi hiyo, mawakili wa Obiang wameituhumu Ufaransa kuwa inaingilia mamlaka ya ndani taifa hilo la Afrika ya Kati.

Hukumu hiyo ni ushindi kwa taasisi ya kimataifa ya Ufaransa ya uwazi na shirika ya Sherpa ambayo yalifungua malalamiko dhidi ya Nguema.

Mbali na familia ya Nguema aliyekaa madarakani kwa miaka 38, waendesha mashtaka pia wanachunguza familia ya Rais wa zamani wa Gabon, Omar Bongo na familia ya Dennis Sasou Nguesso wa Jamhuri ya Congo.