rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Marekani AU Ethiopia Sudani Kusini DRC Nikki Haley

Imechapishwa • Imehaririwa

Balozi wa Marekani kuzuru Afrika juma lijalo

media
Balozi wa Marekani kwenye umoja wa mataifa Nikki Haley April 3, 2017 New York Drew Angerer / GETTY IMAGES NORTH AMERICA / AFP

Balozi wa Marekani Nikki Haley atakuwa kiongozi wa ngazi ya juu wa Marekani kutembelea Afrika juma lijalo wakati atakapo zuru Sudan Kusini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Ethiopia.


Haley atakutana na viongozi kutoka Umoja wa Afrika huko Addis Ababa siku ya Jumatatu kabla ya kwenda Juba na Kinshasa kwa ajili ya mazungumzo na viongozi na kukutana na askari wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa, imesema taarifa ya Marekani.

Haley atashuhudia operesheni za Umoja wa Mataifa zinazofanya kazi ya kukabiliana na migogoro na uharibifu katika nchi hizi, ikiwa ni pamoja na ziara na wajumbe wa misaada na maeneo ya uhifadhi wa amani ya Umoja wa Mataifa na mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa kutoa msaada wa uokoaji wa maisha imesema taarifa hiyo hapo jana

Rais Donald Trump alitangaza ziara ya Haley barani Afrika mwezi uliopita wakati wa mkutano na viongozi wa Kiafrika kando ya kikao cha Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa huko New York.

Trump aliwaambia viongozi wa Kiafrika kuwa anasumbuliwa sana na unyanyasaji unaoendelea nchini Sudan Kusini na Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo" lakini alisema amani na mafanikio yatakuja kupitia mchakato unaongozwa na Afrika.

Katika ziara hiyo Haley, amesema, atajadili utatuzi wa migogoro na "muhimu zaidi, kuzuia"migogoro hiyo.

Miezi tisa tangu aingie madarakani Trump ameonesha kuvutiwa kidogo na masuala ya Afrika na ziara ya Haley ni fursa ya kwanza kwa utawala wake kuunda sera yake kuelekea bara hilo.