Pata taarifa kuu
TOGO-MAANDAMANO-USALAMA

Togo yaendelea kukumbwa na maandamano ya upinzani

Polisi wa kupambana na ghasia nchini Togo, walitumia risasi na moto na mabomu ya kutoa machozi kuwasambaratisha waandamanaji wa upinzani hapo siku ya Alhamisi.

Mji mkuu wa Togo, Lome, ulikumbwa na maandamano yenye vurugu Jumatano Oktoba 18.
Mji mkuu wa Togo, Lome, ulikumbwa na maandamano yenye vurugu Jumatano Oktoba 18. REUTERS/via Reuters TV
Matangazo ya kibiashara

Waandamanaji saba walijeruhiwa katika maeneo mbalimbali nchini humo.

Upinzani umesema kuwa watu wanne waliouawa kwa kupigwa risasi na polisi, madai ambayo yamekanushwa na polisi.

Lengo la maandamano haya ni kushinikiza kumalizika kwa uongozi wa miaka 50 wa familia ya rais wa nchi hiyo Faure Gnassingbe lakini pia wanapinga kubadilishwa kwa katiba kwa lengo la kumsaidia rais wa sasa kuendelea kukaa madarakani.

Hata hivyo upinzani umeapa kuendelea na maandamano, huku ukishtumu polisi kutumiwa na chama tawala kwa kusababisha vifo na vurugu nchi nzima.

Upinzani umeomba vyombo vya sheria kuwafikisha mahakamani polisi waliohusika na vifo vya waandamanaji nchini humo.

Wakati huo huo Ufaransa, kupitia Waziri wa Mambo ya Nje umewataka wananchi wa Togo kuwa watulivu na kuzitaka pande zinazohasimiana kufikiria usalama wa taifa la Togo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.