Pata taarifa kuu
CAR-UN-USALAMA

Antonio Guterres aamuru kutumwa kwa askari 900 Jamhuri ya Afrika ya Kati

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, ameamuru kuimarisha kikosi cha kulinda amani nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati (Minusca) kwa kuongeza idadi ya askari 900 kutokana na kuzuka upya kwa machafuko nchini humo.

Antonio Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa aonya dhidi ya ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Antonio Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa aonya dhidi ya ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati. DR
Matangazo ya kibiashara

Katika ripoti iliyowasilishwa siku ya Jumanne kwa Baraza la Usalama, Bw. Guterres anasema Jamhuri ya afrika ya Kati inatisha kwa sasa .

"Ni kweli kuwa hali ya usalama ilizorota katika miezi ya hivi karibuni, hasa kusini mashariki, na hali hiyo inaweza kusababisha hali ya usalama inazidi kuwa mbaya licha ya jitihada nyingi zilizofanywa ili kuepuka kuongezeka kwa mgogoro," Antonio Guterres amebaini katika ripoti yake hiyo.

"Hali ya kibinadamu nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati inatia wasiwasi," ameongeza Antonio Guterres ambaye hivi karibuni atazuru nchi hiyo, ziara yake ya kwanza tangu alipochukua hatamu ya uongozi mnamo mwezi Januari. Muda wa Minusca unamalizika mwezi Novemba.

Kutokana na hali hii, "ninaamuru kuongezwa kwa askari 900 kwa Minusca", ambayo kwa sasa ina zaidi ya askari 10,000 , Bw. Guterres amesema katika ripoti hiyo iliyowasilishwa kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Wakati huo huo Umoja wa Mataifa unasema watoto nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati wanakabiliwa na baa la njaa na kusababisha kupoteza maisha.

Hatua hii imekuja baada ya machafuko kuendelea kushuhudiwa nchini humo na kusababisha wafanyakazi wa misaada ya kibinadamu kukimbia nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.