Pata taarifa kuu
LIBERIA-UCHAGUZi-SIASA

Uchaguzi wa urais Liberia: Kuelekea duru ya pili Weah-Boakai kuchuana

Liberia inaelekea duru ya pili ya uchaguzi wa urais, ambapo nyota wa zamani wa soka George Weah atachuana na Makamu wa rais Joseph Boakai.

Wafuasi wa chama cha CDC cha George Weah wanafuata zoezi la kuhesabu kura ya duru ya kwanza ya uchaguzi wa urais mjini Monrovia tarehe 13 Oktoba 2017. George Weah na Joseph Boakai watachuana katika duru ya pili, Tume ya Uchaguzi ilitangaza tarehe 15 Oktoba
Wafuasi wa chama cha CDC cha George Weah wanafuata zoezi la kuhesabu kura ya duru ya kwanza ya uchaguzi wa urais mjini Monrovia tarehe 13 Oktoba 2017. George Weah na Joseph Boakai watachuana katika duru ya pili, Tume ya Uchaguzi ilitangaza tarehe 15 Oktoba CRISTINA ALDEHUELA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa matokeo yaliyotangazwa siku ya Jumapili jioni na Tume ya Uchaguzi kulingana na 95% ya kura zilizohesabiwa, nyota wa zamani wa PSG alichukua nafasi ya kwanza kwa 39% ya kura, mbele ya Makamu wa rais Joseph Boakai ambaye amepata 29% ys kura.

Duru ya pili kati ya wawili hao inatarajiwa mnamo mwezi Novemba.

Matokeo yaliyotangazwa na Tume ya Uchaguzi yanathibitisha kukaribiana kwa wagombea hawa kwa kura zilizohesabiwa siku chache zilizopita.

Sasa hatua ngumu imeanza kwa George Weah, ambaye katika duru ya kwanza ya uchaguzi wa urais wa mwaka 2005, aliongoza kwa pointi 8 mbele ya mshindani wake wakati huo Ellen Johnson Sirleaf ambaye katka duru ya pili alishinda kwa 60% ya kura. Watu wengi wanaona kuwa huenda hali kama hiyo ikatokea katika duru ya pili ya uchaguzi wa urais.

Weah na Boakai wote walikuwa wametabiri kuwa wangeshinda duru ya kwanza.

Joseph Boakai, mwenye umri wa miaka 73, amepewa jina la "Sleepy Joe", kwa sababu mara nyingi huonekana kwenye kamera akisinzia. Ni Makamu wa rais wa Ellen Johnson Sirleaf tangu mwaka 2005.

George Weah anaungwa mkono kisiasa na mbabe wa vita aliye gerezani rais wa zamani Charles Taylor. Mke wa zamani wa Taylor Jiwel Howard, ni mgombea mwenza wa Weah.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.