Pata taarifa kuu
NIGER-MAREKANi-MALI-USALAMA

Niger na Marekani wapoteza askari wao kwenye mpaka wa Mali

Askari wa Marekani na Niger waliuawa na watu wenye silaha kwenye mpaka wa nchi jirani ya Mali. Wauaji kutoka nchini Mali waliendesha shambulio, siku ya Jumatano Oktoba 4, katika kijiji cha Tongo Tongo, Kaskazini mwa jimbo la Tillabery, nchini Niger.

Katika jimbo la Tillabery nchini Niger. (Picha ya zamani).
Katika jimbo la Tillabery nchini Niger. (Picha ya zamani). RFI/Sayouba Traoré
Matangazo ya kibiashara

Askari wa kikosi cha Usalama na Upelelezi nchini Niger (BSR) waliendesha operesheni ya kuwasaka watu hao lakini walijikuta wanashambulia. Idadi ambayo si rasmi, askari waliouawa ni wengi. Askari wengi wa Niger na Marekani waliuawa katika shambulio hilo na wengine hawajulikani walipo.

Baadhi ya maafisa wa usalama nchini Niger wamethibitisha kwamba wanajeshi wa watatu wa Marekani wameuawa na wengine wawili kujeruhiwa baada ya kuviziwa nchini Niger karibu na mpaka na Mali.

Wanajeshi hao walishambuliwa vikali walipokuwa wakipiga doria.

Jeshi la Marekani limekuwa likitoa mafunzo kwa jeshi la Niger linalopambana na wanamgambo wa kiislamu eno hilo, na dhidi ya tawi la kundi la al-Qaeda kaskazini mwa Afrika.

Rais wa Marekani Donald Trump amejulishwa na mkuu wake wa majeshi John Kelly kuhusu shambulio hilo, kwa mujbu wa msemaji wa Ikulu ya White House, Sarah Sanders.

Majeshi ya Niger na Marekani yanaendesha operesheni kabambe dhidi ya watu hao. Majeshi hayo yanatumia uwezo mkubwa wa kijeshi ikiwa ni pamoja na mashambulizi ya anga. Ndege za kivita za jeshi la Ufaransapia zinatumiwa katika operesheni hiyo.

Kwa miezi kadhaa, eneo lote la mpakani kutoka eneo la 15 hadi eneo la 19 limewekwa chini ya hali ya dharura. Jeshi la Nigeria lilikuwa na mamlaka kamili ya kurejesha amani kaskazini mwa mikoa ya Tillabery na Tahoua.

Shambulio hiulo linatokea wiki chache tu tangu kuanza kwa operesheni kabambe la kikosi cha kikanda cha G5 Sahel dhidi ya makundi ya wanamgambo wa Kiislamu. Kwa mujibu wa watazamaji kadhaa, kuuawa kwa askari wa Marekani kunaweza kusababisha serikali ya Marekaniinalegeza msimamo wake juu ya kufadhili kikosi hiki cha G5 Sahel.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.