Pata taarifa kuu
SOMALIA-AL SHABAB-USALAMA

Al Shabab yatekeleza shambulizi dhidi ya kambi ya jeshi Somalia

Wanamgambo wa kundi la Al Shabab wameishambulia kambi ya jeshi katika mji wa Barire magharibi mwa mji mkuu Mogadishu, kwa mujibu wa mashahidi.

Kundi la Al Shaba linaendelea kusababidsha uharibifu nchini Somalia.
Kundi la Al Shaba linaendelea kusababidsha uharibifu nchini Somalia. REUTERS/Feisal Omar
Matangazo ya kibiashara

Kundi la Alshabaab limekiri kuhusika na shambulio hilo na limeeleza kwamba liliidhibiti kambi ya jeshi la Somalia na kufanikiwa kuwaua wanajeshi kadhaa. Lakini maafisa wa usalama wamekanusha madai hayo ya Al Shabab.

Shambulio hilo limetokea Ijumaa alfajiri na wakaazi wanasema waliamshwa kwa sauti za milipuko miwili mikubwa.

Wakati huo huo watu saba wameuwa na wengine kujeruhiwa mjini Mogadishu nchini Somalia baada ya gari lililokuwa limetegewa bomu kulipuka.

Mlipuko huo ulitokea karobu na soko kubwa hapo jana.

Al Shabab imeendelea kukabiliana na serikali ya Mogadishu kwa lengo la kuiangusha serikali hiyo inayoungwa mkono na Jumuiya ya Kimataifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.