Mamia ya raia wa Togo wakimbilia Ghana
Mamia ya raia wa Togo wamekimbilia nchi jirani ya Ghana kwa kuhofia kukamatwa na maafisa wa serikali. Hali ya wasi wasi inaendelea kuripotiwa nchini humo
Imechapishwa:
Hatua hii imekuja kwa sababu ya maandamano yanayoendelea hasa jijini Lome, kushinikiza mabadiliko ya Katiba na kumalizika kwa uongozi wa rais Faure Gnassingbe.
Maandamano wa upinzani yanatarajiwa kuendelea leo na mengine yanatarajiwa kufanyika kesho.
Upinzani umtuhumu rais Faure Gnassingbe na Serikali yake kwa kupindisha kweli na kukwepa uhalisia wa wito wanaoutoa kuhusu kufanyika kwa mabadiliko ya katiba ya nchi hiyo.
Muungano huu wa vyama 14 vya upinzani unataka kuwepo kwa mihula miwili ya rais na kuwekwa kwa mifumo miwili ya upigaji kura.
Upinzani umeitisha maandamano makubwa ya nchi nzima kushinikiza kuondoka madarakani kwa Serikali ya rais Gnassingbe.