Pata taarifa kuu
TOGO-MAANDAMANO-USALAMA

Upinzani nchini Togo watoa wito kwa maandamano makubwa

Vyama vya upinzani nchini Togo vimetangaza kuahirisha mazungumzo kuhusu mabadiliko ya katiba na badala yake sasa wametaka kufanyika kwa maandamano makubwa kuipinga serikali.

Upinzani wafanya maandamano mjini Lomé, Togo, wakimtaka  rais Faure Gnassingbe kuachia ngazi, tarehe 6 Septemba 2017.
Upinzani wafanya maandamano mjini Lomé, Togo, wakimtaka rais Faure Gnassingbe kuachia ngazi, tarehe 6 Septemba 2017. REUTERS/Noel Kokou Tadegnon
Matangazo ya kibiashara

Kwenye taarifa yao wapinzani wanamtuhumu rais Faure Gnassingbe na Serikali yake kwa kupindisha kweli na kukwepa uhalisia wa wito wanaoutoa kuhusu kufanyika kwa mabadiliko ya katiba ya nchi hiyo.

Muungano huu wa vyama 14 vya upinzani unataka kuwepo kwa mihula miwili ya rais na kuwekwa kwa mifumo miwili ya upigaji kura.

Awali vyama vya upinzani vilikuwa vikutane Ijumaa ya wiki hii kuzungumzia mabadiliko haya lakini badala yake wameitisha maandamano makubwa ya nchi nzima kushinikiza kuondoka madarakani kwa Serikali ya rais Gnassingbe.

Wiki iliyopita Serikali ilikubali kupeleka muswada bungeni wa kujadiliwa kwa mabadiliko ya katiba lakini hata hivyo juma hili wakati wa vikao vya bunge ajenda hiyo iliondolewa na kuamsha hasira toka kwa upinzani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.