Pata taarifa kuu
COTE D'IVOIRE-USALAMA-HAKI

Wafungwa 100 watoroka jela la Katiola, Cote d'Ivoire

Karibu wafungwa 100 wametoroka jela nchini Cote d'Ivoire. Haijaffahamika ikiwa kulikuwa na makabiliano yoyote baada ya kutokea kwa tukio hili.

Kituo cha polisi cha  Katiola kilichomwa moto wakati wa makabiliano ya Oktoba 3, 2017.
Kituo cha polisi cha Katiola kilichomwa moto wakati wa makabiliano ya Oktoba 3, 2017. STRINGER / AFP
Matangazo ya kibiashara

Ripoti zinasema kuwa wafungwa hao walitoroka katika ndani ya jela ya mji wa Katiola katikati ya nchi hiyo, wakati milango ilipofunguliwa ili wafanye usafi.

Kituo cha taifa nchini humo kineleza kuwa wafungwa hao wanatafutwa lakini tayari 10 wameshakamatwa.

Kisa hiki kinatokea baada ya wafungwa wengine 20 kutoroka jela jijini Abidjan, baada ya kuwavamia maafisa wa usalama.

Nchi ya Cote Dvoire imeendelea kukumbukwa na utovu wa usalama hasa ndani ya jela na miezi ya hivi karibuni ndani ya jeshi baada ya baadhi ya maafisa kugoma na kufanya maandamano.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.