Pata taarifa kuu
GAMBIA-KENYA-UCHAGUZI

Kufutwa kwa uchaguzi wa Kenya imekua ni gumzo nchini Gambia

Siku ya Ijumaa Mahakama Kuu ya Kenya iliamua kufuta uchaguzi wa urais kutokana na makosa. Tukio hili linagonga vichwa vya habari katika magazeti mengi nchini Gambia, ambapo uchaguzi wa urais nchini ulikumbwa na hali inayotaka kufanana na hii inayoshuhudiwa nchini Kenya.

Kwa upande wa wanaharakati wa mabadiliko nchini Gambia, uchaguzi nchini Kenya ni ishara kwamba siasa imeanza kubadilika barani Afrika (picha: soko la Serrekunda mjini Banjul).
Kwa upande wa wanaharakati wa mabadiliko nchini Gambia, uchaguzi nchini Kenya ni ishara kwamba siasa imeanza kubadilika barani Afrika (picha: soko la Serrekunda mjini Banjul). RFI/Guillaume Thibault
Matangazo ya kibiashara

Mwezi Desemba mwaka jana, Rais Yahya Jammeh, baada ya miaka 22 madarakani, alipoteza kura dhidi ya mpinzani wake Adama Barrow. Kwa upande wa wanaharakati wa mabadiliko nchini Gambia wanasema uchaguzi huu uliyo washangaza wengi nchini Kenya ni ishara kwamba siasa imeanza kubadilika barani Afrika.

Tangu Mahakama Kuu kutangaza siku ya Ijumaa (Septemba 1), Wagambia wengi wamekua wakifuata kwa karibu yale yanayojiri nchini Kenya, kama vile Marr Nyang, mwanaharakati kijana aliyeshiriki katika mashirika kadhaa yaliyopigania mabadiliko nchini Gambia. Kile kinachotokea nchini Kenya kwake ni ishara kwamba mabadiliko yameanza kuonekana barani Afrika. "Tunaona Afrika mpya inaanza kujikomboa. Gambia ilikuwa ya kwanza, na Kenya inatafuta njia ile ile, "alisema. Kile Mahakama Kuu ilifanya nchini Kenya ni kitu ambacho Waafrika wanapaswa kujifunza. Na nadhani kwamba wakati Gambia iiliingia katika mchakato huu wa kidemokrasia, hali hii pia ilifungua akili za Waafrika wengi. "

Salieu Taal, mwanzilishi wa vuguvugu liitwalo La Gambia, amesema kile kilichotokea Kenya kimempa shauku kubwa, mpaka aliposikia rais wa Kenya akiwakosoa majaji wa Mahakama Kuu: "Nilivutiwa sana wakati Uhuru Kenyatta alitangaza kwa mara ya kwanza kwamba aliheshimu uamuzi wa Mahakama Kuu, ni hatua kubwa kwa Afrika. Lakini alirudi kwa maneno yake na kusema kuwa majaji hawakuheshimu matakwa ya wananchi. Ni aibu. "

Essa Njie pia ni mwanaharakati na mhadhiri katika sayansi ya siasa katika Chuo Kikuu, naye pia amesema: "Wagambia wanaweza kujifunza kutoka kwa kile kilichotokea nchini Kenya. "Taasisi zetu zinahitaji kuimarishwa. Na mara vyombo vyetu vya sheria vitakua huru, itawezekana kuwa uchaguzi uliyofanyika utatangazwa umefitwa, : Essa Njie amesema, huku akibaini kwamba hali hiyo inathibitisha kuwa taasisi zetu zina nguvu. "

Wote wanasubiri uchaguzi mpya, ndani ya siku 60, wakitumaini kuwa utafanyika kwa utulivu na amani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.