Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-ZIMBABWE-MUGABE

Mashirika ya kiraia kuomba Grace Mugabe aondolewe kinga

Shirika la wanaharakati nchini Afrika Kusini, Afriforum, limetangaza Jumatatu hii Agosti 2 nia yake ya kuwasilisha maombi yake mbele ya mahakama ya kutaka mkewe rais wa Zimbabwe Robert Mugabe aondolewe kinga ya kidiplomasia iliyotolewa na serikali ya Afrika Kusini.

Rais Robert Mugabe na mke wake Grace Mugabe wakihudhuria mkutano wa chama chake cha ZANU (PF) katika eneo la Chinhoyi, Zimbabwe, Julai 29, 2017.
Rais Robert Mugabe na mke wake Grace Mugabe wakihudhuria mkutano wa chama chake cha ZANU (PF) katika eneo la Chinhoyi, Zimbabwe, Julai 29, 2017. REUTERS/Philimon Bulawayo
Matangazo ya kibiashara

Grace Mugabe anashtumiwa kumshambulia Gabriella Engels mjini Johannesburg, nchini Afrika Kusini.

"Tutaomba mahakama kusema kwamba uamuzi wa wa kumpa mkewe rais `mugabe kinga ya kidiplomasia ni kinyume cha sheria kwa sababu, kulingana na sheria yetu, kinga ya kidiplomasia haiwezi kutumika katika kesi kubwa ya uhalifu na unyanyasaji" Kallie Kriel, kiongozi wa Afriforum ameliambia shirika la habari la AFP.

Grace Mugabe alirudi Zimbabwe licha ya kutafutwa na polisi Afrika Kusini.

Mapema siku ya Jumapili jioni vyombo vya habari nchini Zimbabwe vilisema mkewe rais Mugabe, Grace Mugabe alirejea nyumbani kutoka Afrika kusini licha ya kukabiliwa na mashtaka ya kushambulia mwanamitindo Gabriella Engels katika hoteli moja Johannesburg.

Inaeleweka kwamba Grace Mugabe alisafiri pamoja na mumewe siku ya Jumapili asubuhi.

Wawili hao walikuwa wanahudhuria mkutano wa kikanda Afrika kusini.

Mawakili wa Gabriella Engels mwanamke ambaye analaumu Bi Mugabe kwa kumgonga, wanasema kuwa mteja wao alipewa pesa kuachana na kesi hiyo lakini akakataa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.