Pata taarifa kuu
DRC

Idadi ya vifo kutokana na maporomoko ya ardhi DRC huenda ikaongezeka

Idadi ya watu ambao wamepoteza maisha kufuatia maporomoko ya ardhi kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Demokrasi ya Congo, huenda ikapanda hadi kufikia watu 200, maafisa wamesema.

Picha ikionesha athari ya maporomoko ya ardhi nchini Sierra Leone
Picha ikionesha athari ya maporomoko ya ardhi nchini Sierra Leone Reuters/Afolabi Sotunde
Matangazo ya kibiashara

Watu ambao wamepoteza maisha ni kutoka jamii ya wafugaji katika ziwa Albert.

Maafisa wanasema kuwa idadi hiyo ni kutokana na idadi ya familia zilizofukiwa baada ya mvua kubwa kusababisha sehemu za mlima ulio karibu kuporomoka.

Naibu gavana wa mkoa wa Ituri amesema matumaini ya kuwapata manusura yamedidimia wakati waokoaji wakiwa hawana njia za kuondoa mawe makubwa.

Janga kama hilo limeikumba pia nchi ya Sierra Leone ambapo zaidi ya watu 400 wamepoteza maisha huku 600 wakiwa hawajulikani waliko.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.