Pata taarifa kuu
SIERRA LEONE-MAFURIKO

Mamia ya watu waliopoteza maisha nchini Sierra Leone wazikwa

Mazishi ya mamia ya raia wa Sierra Leone wanazikwa leo baada ya kupoteza maisha katika mafuriko makubwa na maporomiko ya ardhi jijini Freetown.

Janga la maporomoko ya ardhi na mafuriko nchini Sierra Leone
Janga la maporomoko ya ardhi na mafuriko nchini Sierra Leone Reuters/Afolabi Sotunde
Matangazo ya kibiashara

Janga hilo lilisababishwa na mvua kubwa ambayo imekuwa ikinyesha katika jiji hilo na mbali na vifo hivyo, mali ya Mamilioni ya fedha imeharibika.

Wizara ya afya inasema tayari watu wengine 400 wameshazikwa baada ya wapendwa wao kuwatambua.

Watoto 100 nao wamethibitishwa kuwa miongoni mwa watu waliopoteza maisha katika janga hili.

Mazishi haya yanafanyika wakati huu, kukiwa na hofu ya watu wengine 600 ambao bado hawajapatikana na kuzua wasiwasi kuwa idadi ya vifo itaongezeka.

Janga hili limezua huzuni kubwa nchini humo huku rais Ernest Bai Koroma akitoa wito kwa wahisani kujitokeza kuwasaidia waathiriwa wa janga hilo.

Umoja wa Mataifa pia imetaka kusaidiwa kwa maelfu ya watu waliopoteza mali zao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.