Pata taarifa kuu
ZAMBIA-SIASA-HAKI

Polisi yamshikilia mwanasiasa mwengine wa upinzani Zambia

Polisi nchini Zambia wanamshikilia kiongozi mmoja wa chama kidogo cha upinzani cha United Progressive Party (UPP) Savior Chishimba, ambaye ameonekana kuwa mkosoaji numba mbili wa Rais Edgar Lungu.

Kiongozi mkuu wa upinzani nchini Zambia Hakainde Hichilema akiambatana na mwanae Habwela Hakainde, kabla hajafungwa. (Picha ya zamanni).
Kiongozi mkuu wa upinzani nchini Zambia Hakainde Hichilema akiambatana na mwanae Habwela Hakainde, kabla hajafungwa. (Picha ya zamanni). REUTERS/Jean Serge Mandela
Matangazo ya kibiashara

Bw Chishimba alikamatwa siku ya Alhamisi punde baada ya kukamilishwa mahojiano ya moja kwa moja kwenye studio ya kituo cha televisheni binafsi mjini Lusaka.

Huyu atakuwa ni mpinzani wa pili kukamatwa baada ya kinara wa upinzani nchini humo Hakainde Hichilema, hatua inayochukuliwa na wanaharakati kuwa ni njama za kutaka kuuminya upinzani nchini humo.

Hivi karibu Hichilema alisema kwa kipindi chote hicho amekuwa akipitia kipindi kigumu kwa sababu haki zake msingi  zinakiukwa na amezuiwa katika mazingira mabaya.

Hichilema alikamatwa mapema mwaka huu baada ya msafara wake kuzuia msafara wa rais Edgar Lungu.

Mwanasiasa huyo ameyakanusha madai hayo na kusema ni ya kisiasa yanayotumiwa dhidi yake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.