Pata taarifa kuu
LIBYA-USALAMA-SIASA

Mahasimu wawili nchini Libya wakutana

Katika mkutano wa siku ya Jumanne Julai 25 uliofanyika katika mji wa La Celle-Saint-Cloud, karibu na Paris, mahasimu wawili nchini Libya, Fayez al-Sarraj na Khalifa Haftar walipitisha taarifa ya pamoja ya kumaliza mgogoro nchini Libya.

Waziri Mkuu wa Libya Fayez al-Sarraj (kushoto) na Jenerali Khalifa Haftar, mkuu wa kikosi kiitwacho Libya National Army (NLA), wakipeana mkono mbele ya rais wa Ufaransa Emmanuel Macron katika mji wa Celle-Saint-Cloud, karibu na paris, Julai 25, 2017.
Waziri Mkuu wa Libya Fayez al-Sarraj (kushoto) na Jenerali Khalifa Haftar, mkuu wa kikosi kiitwacho Libya National Army (NLA), wakipeana mkono mbele ya rais wa Ufaransa Emmanuel Macron katika mji wa Celle-Saint-Cloud, karibu na paris, Julai 25, 2017. REUTERS/Philippe Wojazer
Matangazo ya kibiashara

Rais Emmanuel Macron, ambaye alisimamia mkutano huo alikaribisha "ujasiri wa kihistoria" wa viongozi hawa wawili wenye nguvu nchini Libya na alitangaza makubaliano kwa ajili ya mchakato wa uchaguzi "katika majira ya baridi."

Nakala hii ni ya makubaliano ya yale yatakayotekelezwa nchini Libya ambayo yalipitishwa, wakati wa mkutano ulisimamiwa na Ufaransa pamoja na Umoja wa Mataifa. Mkataba huu wenye pointi 10, uliopitishwa lakini haujatiwa saini na pande zote mbili katika mgogoro wa Libya unazungumzia utekelezaji wa kusitisha mapigano, ushirikishwaji wapande mbalimbali katika migogoro, kuwaingiza katika jeshi wapiganaji na hasa mchakato wa uchaguzi uliopangwa kufanyika katika maira ya baridi. Taarifa hii imetolewa katika mfumo wa mkataba uliosainiwa katika mji wa Skhirat mwaka 2015, lakini unaweza kufanyiwa marekebisho, taarifa hiyo ilisema.

Fayez al-Sarraj na Khalifa Haftar walipeana mkono mbele ya rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, ambaye baadaye alpewa nafasi ya kuzungumza. "Ujasiri wenu kwa leo ni wa kihistoria," alisema rais wa Ufaransa. "Mengi bado yatafanyika. Uhasama wa kisiasa na kijeshi unaweza kudhoofisha juhudi hizi, "Rais Emmanuel Macron aliongeza, kabla ya kuhitimisha: "Kama Libya inashindwa, ni eneo lote litakua liimeshindwa, nakujiandaa kwa madhara ya moja kwa moja kwa Ulaya."

Ufaransa inatarajia kwamba taarifa hii itaruhusu mapambano dhidi ya ugaidi na biashara haramu. Hayo yanajiri wakati ambapo mapigano bado yanaendelea kurindima nchini Libya. Wahusika wakuu wote wa mgogoro watazingatia taarifa hii.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.