Pata taarifa kuu
JAMHURI YA AFRIKA YA KATI

Rais Touadéra na Spika wa bunge Meckassoua wazozana

Juhudi za maridhiano nchini Jamuhuri ya Afrika ya kati zimeendelea kufifia wakati huu rais wa nchi hiyo Faustin-Archange Touadéra akiendelea kutofautiana na Spika wa bunge Abdoul Karim Meckassoua.

Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati  Faustin-Archange Touadéra
Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Faustin-Archange Touadéra REUTERS/Siegfried Modola/Files
Matangazo ya kibiashara

Rais Touadéra na Spika Meckassoua wameendelea kulaumiana kuingilia majukumu ya taasisi hizo mbili na hivyo kuendeleza mzozo wa uongozi nchini humo.

Mvutano huu wa maneno unaendelea kushuhudiwa wakati huu makundi ya waasi ya Anti Balaka na Seleka yakiendelea kupambana katika maeneo mbalimbali nchini humo na kusababisha vifo vya watu na maelfu kuyakimbia makwao.

Mwezi uliopita, mwafaka wa kusitisha mapigano hayo yaliafikiwa mjini Roma nchini Italia baada ya Kanisa Katoliki kufanikiwa kuwaleta pamoja waasi na serikali, lakini mapigano yameendelea kushuhudiwa.

Wakati uo huo, Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia maswala ya watoto UNICEF linalalamikia visa vya watoto kuendelea kutekwa na kupelekwa kusikojulikana.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.