rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Afrika Ethiopia AU Japani

Imechapishwa • Imehaririwa

Benki ya Afrika na Japan zatiliana saini makubaliano kuhusu maendeleo ya nishati

media
Nembo ya Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB logo

Serikali ya Japan na Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB zimetiliana saini makubaliano ya kuazishwa kwa mchakato wa nishati kati ya Japan na Afrika ili kutoa mchango katika makubaliano kuhusu nishati kwa bara la Afrika, ambayo yanalenga kumfanya kila mwananchi kupata nishati ya uhakika ifikapo mwaka 2025 kwa kutumia rasilimali za nishati zilizopo pamoja na teknolojia ya hali ya juu.


Makubaliano haya yalitiwa saini kando na mkutano wa wakuu wa nchi za Afrika uliomalizika hivi karibuni jijini Addis Ababa, Ethiopia.

Kutokana na majadiliano yaliyoanzishwa na viongozi wa Afrika wakati wa mkutano wa 6 wa kimataifa wa Tokyo kuhusu maendeleo ya Afrika, TICAD-VI uliofanyika jijini Nairobi mwaka 2016 na pia ziara ya rais wa benki ya Afrika, Dr Akinwumi Adesima nchini Japan, Serikali ilithibitisha utayari wake wa kusaidia mkakati wa maendeleo ya nishati kati ya Japan na bara la Afrika.

Mchakato huu utachangia pakubwa kwa juhudi za barala Afrika katika kufikia mapengo ya pamoja ya kidunia kuhusu nishati na kubadilisha mifumo yake ya nishati kupitia njia ambazo sio za gharama kwa kuchanganya na matumizi ya nishati mbadala na rasilimali nyingine.

Chini ya mchakato huu beki ya Maendeleo ya Afrika itaongoza mradi wa maendeleo kwa kushauriana na nchi wanachama.

Nchi ya Japan iko tayari kutoa kiasi cha hadi kufikia dola za Marekani bilioni 6 kufadhili miradi ya operesheni ambayo itapeleka umeme majumbani, mashuleni, mahospitalini, kwenye kilimo, viwanda na nishati mbadala za kupikia.

Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Dr Akinwumi Adesina AfDB

Mchakato huu utafadhili shughuli mbalimbali zitakazohusiana na masuala ya uma na yale ya sekta binafsi hasa kuhusu miradi ya nishati, hii ni pamoja na kuandaa ujenzi kupitia mchanganuo mzuri wa fedha na usaidizi wa kiufundi.

Akizungumza kwenye sherehe za utiaji saini makubaliano haya rais wa benki ya Afrika Adesina amesema “napenda kuishukuru Serikali ya Japan kwa usaidizi wao wa muda mrefu kwa AfDB na bara la Afrika. Nakaribisha kwa mikono miwili usaidizi wa nchi ya Japan kwa makubaliano haya kuhusu nishati kwa bara la Afrika”.

Balozi wa Japan nchini Ethiopia Shinichi Saida alisoma ujumbe wa naibu waziri mkuu wa Japan ambaye pia ni waziri wa fedha Taro Aso ambaye alisema ana imani kupitia mchakato huu, nchi yake itachangia pakubwa kufikia malengo na kupeleka umeme kwenye maeneo mengi ya bara la Afrika.

Benki ya Afrika na Serikali ya Japan zitafanya kazi kwa karibu katika kutekeleza makubaliano yenyewe ndani ya majuma machache yajayo na kabla ya mwisho wa mwaka 2017.