Pata taarifa kuu
CAR-USALAMA

CAR yaendelea kukabiliwa na machafuko mbalimbali

Mapigano ya wiki mbili kati ya makundi yenye silaha kwenye mji wa Zemio kusini mwa nchi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati yamesababisha vifo vya watu 6 na maelfu wengine kukimbia makazi yao, hii ni kwa mujibu wa ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa.

Zaidi ya wakimbizi 150,000 walivuka mpaka kati ya Chad na Jamhuri ya Afrika ya Kati katika kipindi cha miezi ya hivi karibuni.
Zaidi ya wakimbizi 150,000 walivuka mpaka kati ya Chad na Jamhuri ya Afrika ya Kati katika kipindi cha miezi ya hivi karibuni. REUTERS/Siegfried Modola
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa makadirio ya awali ya umoja wa Mataifa, inakadiriwa kuwa watu zaidi ya elfu 2 hawana mahali pakuishi kutokana na mapigano haya ambayo pia yameripotiwa kwenye maeneo mengine ya nchi.

Jamhuri ya afrika ya Kati inaendelea kukabiliwa na machafuko, huku raia wakisema wanatiwa na wasiwasi na hali mbaya inayoendelea kushuhudiwa ncini humo.

Machafuko nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati yamesababidsha vifo vya watu, huku maelfu ya raia wakilazimika kuyahama makazi yao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.