Pata taarifa kuu
SENEGAL-SIASA

Rais wa zamani Abdulaye Wade arejea nyumbani kuwania ubunge

Rais wa zamani wa Senegal Abdulaye Wade amerejea nyumbani jijini Dakar kushiriki uchaguzi wa wabunge ambao umepangwa kufanyika tarehe 30 mwezi Julai mwaka huu, ambapo pia anagombea kama mbunge.

Rais wa zamani Abdoulaye Wade akiwasili jijini Dakar baada ya kuondoka nchini Ufaransa.
Rais wa zamani Abdoulaye Wade akiwasili jijini Dakar baada ya kuondoka nchini Ufaransa. Guillaume Thibault / RFI
Matangazo ya kibiashara

Wade mwenye umri wa miaka 91 amesema anaamini kuwa lengo lake kugombea ubunge ni kwa sababu anataka kuendelea kuwatetea raia.

Katika kampeni yake, ameshutumu serikali ya rais Macky Sall iliyoko madarakani kwa kuchochea kesi inayomkabili mtoto wake Karim Wade, ambaye anakabiliwa na kesi ya kujitajirisha kinyume cha sheria.

Wade, aliongoza Senegal kwa miaka 12 kati ya mwaka 2000 hadi mwaka 2012 na kwenda kuishi nchini Ufaransa.

Mwaka 2012, aliwania urais kwa muhula wa wa tatu lakini akashindwa baada raia wa nchi hiyo kumchagua kiongozi wa sasa Macky Sall.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.