rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

CAR HRW

Imechapishwa • Imehaririwa

HRW yaomba kuimarishwa kwa mahakama maalum CAR

media
Bangui, mnamo mwezi Desemba 2014. AFP PHOTO / PACOME PABANDJI

Shirika la kutetea haki za Binadamu la Human Rights Watch, linataka uungwaji mkono wa Mahakama mpya iliyoundwa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati kusikiliza na kuamua kesi mbalimbali za mauaji nchini humo.


Human Rights Watch inasema uugwaji mkono wa Mahakama hii itasaidia sana kupunguza visa vya makundi ya waasi kuwauwa raia wa kawaida lakini pia waathiriwa kupata haki.

Mahakama hiyo maalum inawajumuisha majaji wa nchi hiyo na wale wa kimataifa, pamoja na viongozi wa Mashtaka.

Human Rights Watch inasema, Mahakama hiyo inastahili kupata uungwaji mkono kutoka kwa Umoja wa Mataifa lakini pia kupewa msaada wa kifedha ili kufanikisha kazi yake.

Wakati huo huo, shirika hilo limesema watu 560 wameuawa nchini humo kwa kipindi cha miaka miwili na nusu. Wapiganaji wa  makundi ya waasi wa Seleka na Anti Balaka wananyooshewa kidole cha lawama kuhusika katika mauaji hayo.