Pata taarifa kuu
SUDAN-UN

Azimio la UN Kupunguza walinda amani Sudan lapitishwa

Serikali ya Sudan inasema uamuzi wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kupunguza idadi ya wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja huo jimboni Darfur, ni wa mwisho.

Wajumbe wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa wakipiga kura.
Wajumbe wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa wakipiga kura. UN Photo/Loey Felipe
Matangazo ya kibiashara

Wiki hii Baraza hilo lilikubali kupunguza idadi ya wanajeshi hao wanaowashirikisha pia wale kutoka barani Afrika UNAMID kwa asilimia 30.

Mwaka 2007, Umoja wa Mataifa ulituma wanajeshi 16,000 kwenda kuwalinda raia katika jimbo la Darfur baada ya kuzuka kwa makabiliano makali kati ya makundi ya wapiganaji na wanajeshi wa Sudan kuanzia mwaka 2003.

Umoja wa Mataifa umekuwa ukisema kuwa watu 300,000 wameuawa na wengine zaidi ya Milioni mbili wameyakimbia makwao na kusalia wakimbizi kutokana na mapigano hayo.

Makabila madogo yameunga makundi ya waasi kupambana na serikali ya Khartoum ambayo inaongozwa na watu wenye asili ya kiarabu, wanaodaiwa kuwabagua.

Serikali ya Khartoum imekuwa ikisema mapigano katika jimbo hilo yameisha lakini mapigano yameendelea kuripotiwa hivi karibuni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.