Pata taarifa kuu
MALI

Wanajihadi watano wauawa jijini Bamako nchini Mali

Maafisa wa usalama nchini Mali wanasema limewauwa wanajihadi watano waliohusika na shambulizi na uvamizi wa kituo cha kitalii jijini Bamako mwishoni mwa juma lililopita.

Eneo la kitalii la  Kangaba, jijini Bamako nchini Mali lililovamiwa na wanajihadi.
Eneo la kitalii la Kangaba, jijini Bamako nchini Mali lililovamiwa na wanajihadi. REUTERS/ REUTERS TV
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa usalama Salif Traore amethibitisha kutokea kwa mauaji hayo na kusema shambulizi lililotokea lilikuwa ni la kigaidi.

Maafisa wa usalama wamesema walikabiliana na wanajihadi hao usiku kucha na hatumaye kufanikiwa kuwadhibiti.

Traore ameongeza kuwa maafisa wa usalama walifanikiwa kuwaokoa wageni 30 waliokuwa katika kituo hicho.

Mkuu wa sera za mambo ya nje ya Umoja wa Ulaya Federica Mogherini, amesema watalii wawili kutoka barani Ulaya walipoteza maisha katika tukio hilo.

Licha ya jeshi la Ufaransa kwenda nchini Mali mwaka 2013, kuisaidia serikali ya Bamako kupambana na makundi ya kijihadi, nchi hiyo imeendelea kukabiliwa na mashambulizi ya kigaidi mara kwa mara.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.