Pata taarifa kuu
UFARANSA-IVORY COAST-SENEGAL

Ufaransa: Rais Macron akutana na Rais Ouattara wa Ivory Coast, baadae kukutana na rais wa Senegal

Ufaransa na Ivory Coast wataongeza ushirikiano wa kijeshi na kubadilishana taarifa za kiintelijensia katika wiki chache zijazo hatua inayolenga kushinda vita dhidi ya ugaidi kwenye nchi za Afrika Magharibi.

Rais wa Ivory Coast Alassane Ouattara akisalimiana na mwenyeji wake rais wa Ufaransa Emmanuel Macron. Juni 11, 2017
Rais wa Ivory Coast Alassane Ouattara akisalimiana na mwenyeji wake rais wa Ufaransa Emmanuel Macron. Juni 11, 2017 REUTERS/Mal Langsdon
Matangazo ya kibiashara

Haya yamekubaliwa katika mazungumzo kati ya rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na rais wa Ivory Coast Alassane Ouattara ambaye yuko nchini Ufaransa kwa ziara ya kikazi ambapo awali alikutana na waziri wa uchumi.

Rais Ouattara ameahidi nchi yake kutoa mchango wake katika vita dhidi ya ugaidi kwenye mataifa ya Afrika Magharibi.

Mwaka 2016 katika shambulio ambalo kundi la kigaidi lililotekelezwa na wapiganaji wa Al-Qaeda (AQIM) liliua watu 19 kwenye fukwe moja ya Grand Bassam jirani na mji mkuu wa Abidjan.

Rais Ouattara pia alisisitiza kuhusu nia ya nchi yake kuhakikisha uchumi wake unakua kwa asilimia 7 ambapo amesema malengo yao ni kujikita kwenye nishati mbadala na elimu huku akikaribisha na kuunga mkono mkataba wa mabadiliko ya tabia nchi wa Paris.

Kiongozi huyo akamshukuru pia rais Macron kwa mchango wa nchi yake kuipigia kura kuwa mwanachama ambae sio wa kudumu kwenye baraza la usalama la umoja wa Mataifa kuanzia mwaka 2018.

Kwa upande wake rais Macron amesema nchi yake itaendelea kufanya kazi kwa karibu na Serikali ya Ivory Coast, nchi ambayo amesema inaendelea kutoa mchango muhimu katika vita dhidi ya ugaidi.

Baadae rais Macron atakutana pia na rais wa Senegal Macky Sall ambaye nae yuko nchini Ufaransa kwa ziara ya kikazi.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.