Pata taarifa kuu
IGAD-SUDAN KUSINI

Asasi za kiraia zataka IGAD imalize mzozo wa Sudan Kusini

Marais na wawakilishi wa serikali kutoka Mataifa ya Afrika Mashariki katika muungano wa IGAD, wanakutana jijin Addis Ababa nchini Ethiopia kujadili hali ya usalama na wakimbizi nchini Sudan Kusini.

Kambi ya  Ngomoromo katika Wilaya ya  Lamwo Kaskazini mwa Uganda, inayowapa hifadhi wakimbizi kutoka Sudan Kusini
Kambi ya Ngomoromo katika Wilaya ya Lamwo Kaskazini mwa Uganda, inayowapa hifadhi wakimbizi kutoka Sudan Kusini REUTERS/Stringer/File photo
Matangazo ya kibiashara

Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn ambaye pia ni Mwenyekiti wa IGAD anaongoza mkutano huo kujaribu kutafuta suluhu ya kuwasaidia maelfu ya raia wa nchi hiyo wanaoteseka lakini pia kumaliza vita nchini humo.

Hata hivyo, rais Salva Kiir alikataa mwaliko wa kushiriki katika mkutano huo na kumtuma Makamu wake Taban Deng Gai.

Ikulu ya Juba imeripoti kuwa rais Kiir ana majukumu mengine muhimu yanayomfanya kutohudhuria mkutano huu.

Mashirika ya kutetea haki za Binadamu na asasi zingine za kiraia kama Enough Project, yanatoa wito kwa IGAD kuanza kufikiria mbinu mpya ya kumaliza vita vinavyoendelea.

Mkurugenzi Mkuu wa asasi hiyo Jon Temin, amesema kuwa mkutamo huu ni muhimu sana na unatoa nafasi kwa IGAD na Jumuiya ya Kimataifa kumaliza kabisa mzozo wa Sudan Kusini.

Mkataba wa amani kati ya rais Kiir na kiongozi wa waasi Riek Machar uliotiwa saini mwaka 2015, ulivunjika na kusababisha kuendelea kwa vita vinavyoendelea hadi sasa.

Rais Kiir mwezi uliopita alizundia mazungumzo ya kitaifa nchini humo na kutangaza kumalizika kwa vita, hata hivyo mapigano yameendelea kushuhudiwa nchini humo.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.