Pata taarifa kuu
LIBYA-USALAMA

Libya yaendelea kukabiliwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe

Jeshi linalounga mkono mamlaka yenye makao yake katika mji wa mashariki wa Tobruk, limetekeleza mashambuliuzi mengi ya anga dhidi ya vikosi waaminifu kwa serikali inayotambulika kimataifa iliyoko katika mji mkuu wa Libya, Tripoli, kwa mujibu wa taarifa kutoka nchini Libya.

Viosi vya usalama waaminifu kwa serikali ya Umoja nchini Libya, katika mji wa Abou Grein, baada ya kutangazwa kudhibitiwa kwa mji huo.
Viosi vya usalama waaminifu kwa serikali ya Umoja nchini Libya, katika mji wa Abou Grein, baada ya kutangazwa kudhibitiwa kwa mji huo. MISRATA TV via REUTERS TV
Matangazo ya kibiashara

Shirika la Human Rights Watch limebaini kwamba, miongoni mwa watu thelathini waliouawa katika eneo hilo walikuwa na majeraha ya risasi vichwani na baadhi ya maiti zilikuwa zimefungwa mikono.

Mashambulizi saba ya anga yameripotiwa kutekelezwa, hasa katika miji ya Hun na Jafra iliyoko Kusini mwa Libya mwishoni mwa juma lililopita nyakati za usiku. Hata hivyo usiku wa Alhamisi wiki iliyopita ulitokea shambulizi la ulipizaji kisasi, shamblizi ambalo liliendeshwa na kikosi cha anga cha LNA.

Mkuu wa Umoja wa Mataifa anaye shughulikia kitengo cha wakimbizi amesema kwamba raia wanaotafuta hifadhi nchini Libya wanapaswa kuondolewa vizuizini na kupewa usaidizi mwingine.

Filippo Grandi, amesema kwamba ameridhishwa na ulinzi unaotolewa na serikali lakini ameshtushwa na hali mbaya waliyonayo wakimbizi na wahamiaji mahali wanakoshikiliwa.

Umoja wa Mataifa kupitia kitengo hicho kinachoshughulika na wakimbizi kimeeleza kwamba kimechukua hatua ya kuonesha uwepo wake na kuweka mipango ya kukabiliana na hali mbaya kutokana na mgogoro huo.

Libya bado inasalia kuwa ndiyo eneo pekee linalotumiwa na wakimbizi kwenda katika nchi walizozidhamiria ikiwemo kwa matumaini ya kwenda barani Ulaya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.