rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Somalia Mohamed Abdullahi Farmajo Uingereza Boris Johnson UN Antonio Guterres

Imechapishwa • Imehaririwa

Jumuiya ya Kimataifa yakubali kuisaidia Somalia

media
Rais wa Somalia Mohamed Abdulahi (kushoto wa kwanza), waziri wa mambo ya nje wa Uingereza Boris Johson (katikati) na katibu mkuu wa UN Anthonio Guterres. 11MAY2017 REUTERS/Hannah McKay

Nchi ya Somalia imefanikiwa kupata uungwaji mkono zaidi kutoka jumuiya ya kimataifa, ambapo wakuu nchi wamekubali kuisaidia nchi hiyo kudhibiti hali ya usalama, kukabiliana na baa la njaa pamoja na kusaidia sekta za kiuchumi kwenye taifa hilo.


Rais mpya wa Somalia Mohamed Abdullahi Mohamed amesifu uungwaji mkono huo akisema ni hatua ya kihistoria kwa taifa la Somalia mara baada ya kushuhudia nchi yake ikitiliana saini makubaliano na Jumuiya ya kimataifa kuisaidia nchi yake.

Rais Farmajo amesema wakati huu wakiianza safari ya kuelekea maendeleo ana imani kuwa Jumuiya ya kimataifa safari hii itatimiza ahadi zake na kutoitenga nchi yake.

Wachambuzi wa mambo wanasema kuwa makubaliano haya yanatoa angalu mwanga kuwa huenda safari hii mambo yakawa tofauti nchini Somali.

Katika hatua nyingine rais wa Somalia akatoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuiondolea nchi yake makataa ya kununua silaha akisema uhaba wa silaha za kisasa kunawapa nguvu wapiganaji wa Al-Shabab.

Haji Kaburu mchambuzi wa siasa za kimataifa hata hivyo ameeleza hofu yake kuhusu ombi hili la Somalia akisema "kutoa silaha ni sawa na kuamsha makundi mengine kujipanga zaidi na pengine vita inaweza isiishe Somalia, cha msingi ni kuwa na mazungumzo na pande zote mbili".

Wakuu wa nchi na mawaziri walioshiriki kwenye mkutano wa hapo jana, wameipongeza Serikali mpya kwa kuonesha nia ya dhati ya kupambana na vitendo vya rushwa ambavyo vimeidhoofisha nchi hiyo na kusababisha nchi wafadhili kupunguza misaada yao.