Pata taarifa kuu
ICC-LIBYA-USALAMA-HAKI

ICC kuwafungulia mashitaka wanaohusika na uhalifu Libya

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ya ICC imesema hali tete ya usalama na kukosekana kwa mazingira salama nchini Libya, imesababisha kuongezeka kwa matukio ya ukiukaji wa haki za binadamu na uvunjifu wa sheria za nchi.

Wahamiaji wamekusanyika katika bandari ya Tripoli (Libya) baada ya meli yao kuzama.
Wahamiaji wamekusanyika katika bandari ya Tripoli (Libya) baada ya meli yao kuzama. AFP/MAHMUD TURKIA
Matangazo ya kibiashara

Mwendesha mashtaka mkuu wa mahakama hiyo Fatou Bensouda ameonya kuhusu kuendelea kushuhudiwa kwa makosa ya uhalifu wa kivita na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu yanayofanywa na pande zinazohasimiana.

Fatou Bensouda amesema timu yake inakusanya ushahidi wa makosa yanayodaiwa kutendwa kwa wahamiaji wanaopitia nchini Libya.

Bensouda amesema matukio haya yanahatarisha taifa hilo kutumbukia kwenye machafuko zaidi ya wenyewe kwa wenyewe.

Fatou Bensuda ameliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwamba Libya imeonekana kuwa soko la usafirishaji haramu wa binadamu ambapo maelfu ya wahamiaji wasio na msaada, wakiwemo wanawake na watoto wamekuwa wakishikiliwa katika maeneo mbalimbali nchini humo.

Amesema vyanzo vya kuaminika vinaeleza kuwa matukio ya mauaji, ubakaji na utesaji yamekuwa ni matendo ya kawaida katika eneo hilo.

Katika hatua nyingine mahakama hiyo inafikiria ikiwa ianzishe uchunguzi au la kuhusu makosa yanayohusu wahamiaji ambapo inasema nchi ya Libya imekuwa kitovu cha biashara haramu ya binadamu.

Miili ya wahamiaji waliokufa maji yagunduliwa kwenye pwani ya Libya,Februari 20, 2017.
Miili ya wahamiaji waliokufa maji yagunduliwa kwenye pwani ya Libya,Februari 20, 2017. Libyan Red Crescent/Handout via REUTERS

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.