Pata taarifa kuu
UFARANSA-UCHAGUZI 2017

Raia wa Ufaransa kwenye nchi za EAC nao wapiga kura kuchagua rais mpya

Raia wa Ufaransa kwenye nchi za ukanda wa Afrika Mashariki wamepiga kura kwenye duru ya pili ya uchaguzi mkuu wa urais ambao unatajwa kuwa wa kuhistoria katika taifa hilo.

Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Malika Berak akipiga kura yake
Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania, Malika Berak akipiga kura yake RFI/Emmanuel Mbando
Matangazo ya kibiashara

Nchini Tanzania zaidi ya wapiga kura 428 raia wa Ufaransa watapiga kura kwenye uchaguzi wa Jumapili hii kuchagua kati ya mgombea mwenye msimamo wa kati Emmanuel Macron na mgombea mwenye msimamo wa kihafidhina Marine Le Pen.

Vito vya kupigia kura nchini humo vimegawanywa katika makundi mawili ambapo jijini Dar es Salaam wapiga kura zaidi ya 300 wanapiga kura kwenye ubalozi wa Ufaransa, huku kituo kingine kikiwa ni jijini Arusha.

Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Malika Berak mara baada ya kupiga kura amesema zoezi limeenda vizuri na wanatarajia raia wengi wa Ufaransa wanaoishi nchini humo watajitokeza kupiga kura.

Msimamizi wa uchaguzi kwenye ubalozi wa Ufaransa ambayepia ni naibu balozi, Blevin Claude, amesema kuwa wametenga vituo viwili nchini Tanzania ili kuruhusu raia wengi zaidi wanaoishi kwenye mikoa mbalimbali nchini humo kupata nafasi ya kupiga kura.

Blevin amesema utaratibu wa upigaji kura unaruhusu pia kwa ndugu kuwapogia kura ndugu zao wengine kwa kupewa kibali maalumu kufanya hivyo, ambapo wakifika kwenye kituo cha kupigia kura wanaonesha nyaraka ya kibali hicho cha kumpigia kura.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.