Pata taarifa kuu
BURKINA FASO-COMPAORE-HAKI

Kesi ya Compaoré na mawaziri wake kusikilizwa mahakamani

Kesi ya serikali iliyopita ya Blaise Compaoré itasikilizwa tena Alhamisi hii asubuhi May 4 katika Mahakama Kuu mjini Ouagadougou. Kesi hii iliyoanzishwa wiki moja iliyopita, iliahirishwa hadi Alhamisi hii Mei 4. Alhamisi iliyopita, mawaziri 25 wa zamani waliripoti mahakamani.

Mawaziri ishirini na tanowa zamani katika serikali ya Compaore watasikilizwa katika Mahakama Kuu mjini Ouagadougou Alhamisi hii, Mei 4, 2017, rais wa zamani wa Burkina Faso hatokuepo.
Mawaziri ishirini na tanowa zamani katika serikali ya Compaore watasikilizwa katika Mahakama Kuu mjini Ouagadougou Alhamisi hii, Mei 4, 2017, rais wa zamani wa Burkina Faso hatokuepo. RFI/Carine Frenk
Matangazo ya kibiashara

Mawaziri sita wanaoishi uhamishoni watahukumiwa licha ya kutokuepo. Rais wa zamani, ambaye anachukuliwa kama waziri wa ulinzi wa zamani ambaye alichukua uraia wa Cote d'Ivoire atahukumiwa pia licha ya kutokuepo.

Viongozi hao wa zamani wanashtumiwa "mauaji ya kukusudia na kula njama kwa kuwapiga na kuwajeruhi kwa kukusudia waandamanaji." Wanafuatiliwa na mahakama kutokana na kuhusika kwao katika ukandamizaji dhidi ya waandamanaji mwezi Oktoba 2014 ambao ulisababisha kuanguka kwa utawala wa Blaise Compaoré.

Mbele ya mahakimu, mawaziri 25 wa zamani watasikilizwa Alhamisi hii Mei 4. Wote wanashtumiwa kwa kuwa waliamua katika kikao cha baraza la mawaziri cha Oktoba 29, 2014, kutoa wito kwa jeshi kukomesha waandamanaji waliokua wakipinga marekebisho ya Katiba.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka, mawaziri walitoa wito wa kwa majeshi kuwafyatulia risasi waandamanaji, na kusababisha vifo vya watu saba na 88 kujeruhiwa.

Kwa mujibu wa chanzo cha mahakama, kesi haitadumu zaidi ya wiki mbili. siku ya kwanza lazima kujitoa na sehemu ya upekee.

chama Compaore tayari kimeshutumu kwamba "kesi hiyo ni ya kisiasa".

Lydia Karambiri, ambaye mumuwe aliuawa siku ya kwanza ya maandamano nchini Burkina Faso..
Lydia Karambiri, ambaye mumuwe aliuawa siku ya kwanza ya maandamano nchini Burkina Faso.. RFI/Carine Frenk

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.