rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Afrika Ethiopia Yoweri Museveni Hailemariam Desalegn

Imechapishwa • Imehaririwa

Wadau kutoka barani Afrika wakutana jijini Addis Ababa kuzungumzia usimamizi wa rasilimali

media
Rasis wa Uganda Yoweri Museveni akiwasilini jijini Addis Ababa na kukaribishwa na mwenyeji wakeHailemariam Desalegn twitter.com/Tanaforum

Baadhi ya viongozi wa sasa na wale wa zamani wa  bara la Afrika na watalaam wengine wanakutana kwa siku mbili jijini Addis Ababa nchini Ethiopia, kuzungumzia namna rasilimali mbalimbali zinavyoweza kulinufaisha bara la Afrika.


Mkutano huu wa siku mbili unazungumzia pia namna ya kuboresha usimamizi wa rasilimali hizo kwa manufaa ya bara la Afrika.

Bara la Afrika linajivunia utajiri wa rasilimali kama mafuta, gesi , dhahabu, shaba miongoni mwa rasilimali nyingine.

Hata hivyo, utajiri huu badala ya kulinufaisha waafrika, umezua machafuko katika mataifa mbalimbali na kuonekana kama  laani.

Huu ni mkutano wa sita unaoongozwa na rais wa zamani wa Nigeria Olusegun Obasanjo kuangalia namna rasilimali hizi zinaweza kuwatajirisha waafrika badala ya   kuyanufaisha mataifa ya kigeni.

Rais wa Uganda Yoweri Museveni na mwenzake wa Liberia Ellen Johnson Sirleaf na Hailemariam Desalegn wanahudhuria mkutano huo.