rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

UNICEF Nigeria Boko Haram

Imechapishwa • Imehaririwa

UNICEF yasema bado Boko Haram inawatumia watoto kutekeleza mashambulizi

media
Nembo ya UNICEF UNICEF

Ripoti ya Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF, linasema katika kipindi cha miezi mitatu mwaka huu, Idadi kubwa ya watoto walitumiwa kufanya mashambulizi 27 ya kujitoa mhanga katika nchi za Nigeria, Niger, Chad na Cameroon.


Idadi hiyo ya mashambulizi ni zaidi ya yale yaliyofanywa katika mwaka mzima wa 2016 ambapo mashambulizi tisa ndiyo yalihusisha watoto.

Aidha ripoti hiyo imeeleza kuwa watoto wengi wanaotumiwa kufanya mashambulizi hayo ni wasichana, wakilenga maeneo ya umma na vizuizi vya kijeshi.

Umoja wa Mataifa umelaani hila na ulazimishaji unaofanywa na kundi hilo la Boko Haram kuwatumia wanawake na watoto kufanya mashambulizi hayo ya mabomu.

Ripoti hiyo inasema watoto wanapaswa kutazamwa kama waathirika wa matukio hayo na sio watenda kosa.

Idadi kubwa ya wasichama Kaskazini mwa Nigeria hawakwendi shuleni kwa sababu ya kutekwa na Boko Haram.