Pata taarifa kuu
GAMBIA-SIASA

Raia wa Gambia hawakujitokeza kwa wingi kuwachagua wabunge

Raia wa Gambia hawakujitokeza kwa wingi kushiriki katika uchaguzi wa wabunge siku ya Alhamisi.

Rais Adama Barrow akishiriki katika Uchaguzi wa wabunge Aprili 6 2017
Rais Adama Barrow akishiriki katika Uchaguzi wa wabunge Aprili 6 2017 RFI/Claire Bargeles
Matangazo ya kibiashara

Vyombo vya Habari nchini Gambia vimeripoti kuwa idadi kubwa ya wapiga kura hawakujitokeza kushiriki katika zoezi hilo ikilinganishwa na ule wa urais mwaka uliopita.

Waangalizi wa ndani na wale wa Kimataifa wanasema kuwa, katika historia ya uchaguzi nchini humo hii ndio mara ya kwanza kwa Wagambia kutojitokeza kwa wingi.

Wachambuzi wa siasa wanasema kuwa raia wengi wa Gambia, wanaona hakuna haja ya kupiga kura kwa sababu kiongozi wa zamani Yahya Jammeh ameondoka nchini humo.

Hata hivyo, ripoti zinasema kuwa muungano wa chama cha upinzani UDP umepata karibu asilimia 50 ya viti vya ubunge nchini humo sawa na wabunge 31 katika bunge hilo la wabunge 53.

Wapiga kura wa Gambia 880,000 walitarajiwa kushiriki  katika uchaguzi huo uliofanyika kwa mara ya kwanza tangu kuondolewa kwa Jammeh mwaka uliopita.

Katiba ya Gambia inampa mamlaka rais wa nchi hiyo kuteuwa wabunge wengine watano, na hivyo kulifanya bunge la nchi hiyo kuwa na wabunge 58.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.