rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Ufaransa François Hollande Mali

Imechapishwa • Imehaririwa

Mwanajeshi wa Ufaransa auawa nchini Mali katika mapigano na waasi

media
Wanajeshi wa Ufaransa wakipiga doria nchini Mali wordpress.com

Mwanajeshi wa Ufaransa ameuawa usiku wa kuamkia siku ya Alhamisi nchini Mali.


Ripoti zinasema kuwa, mauaji haya yalijiri baada ya wanajeshi wa Ufaransa kukabiliana na waasi Kusini Mashariki mwa nchi hiyo.

Ikulu ya Ufaransa, Elysee, imethibitisha kifo cha mwanajeshi huyo.

Rais Francois Hollande amesema  mwanajeshi huyo anayefahamika kama Julien Barbe, amepoteza maisha akipigania usalama na amani nchini Mali, na anasalia kuwa shujaa.

Ufaransa imekuwa ikiongoza operesheni maarufu kama Serval, kuanzia mwaka 2012 kukabiliana na makundi ya waasi hasa Kaskazini mwa nchi hiyo.

Wanajeshi 17 wa Ufaransa nchini Mali katika makabiliano na waasi nchini Mali.

Mauaji haya yanakuja wakati huu Waziri Mkuu Bernard Cazeneuve akizuru nchini Algeria na baadaye Tunisia.

Naye Waziri wa Mambo ya nje Jean-Marc Ayrault anazuru Mauritania.