Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI

Uongozi wa ANC wasema hautamshinikiza rais Zuma kujiuzulu

Uongozi wa chama tawala nchini Afrika Kusini ANC umesema hauungi mkono mpango wowote wa kumwondoa madarakani rais Jacob Zuma.

Rais Jacob Zuma akionekana mwenye furaha
Rais Jacob Zuma akionekana mwenye furaha REUTERS/Rogan Ward
Matangazo ya kibiashara

Chama hicho kupitia Katibu Mkuu Gwede Mantashe  kimesema baada ya kusikiliza malalamishi kutoka kwa baadhi ya viongozi na wafuasi wa chama tawala, uongozi wa juu haujaona sababu zozote za msingi za kumshinikiza Zuma kuachia madaraka.

Kufutwa kazi kwa Waziri wa Fedha Pravin Gordhan wiki iliyopita kumeonekana kukigawa chama hicho.

Hatua hii ni faraja kubwa sana kwa rais Zuma ambaye amekuwa akipata shinikizo za kujiuzulu baada ya kufanya uamuzi huo lakini pia kushutumiwa kujihusisha na ufisadi, madai ambayo amekanusha.

Zuma ambaye ni Mwenyekiti wa chama cha ANC, anaweza kupoteza nafasi hiyo na hivyo kupoteza urais ikiwa uongozi wa juu utaamua kumpokonya nafasi hiyo kwa mujibu wa Katiba wa chama hicho.

Mwaka 2008, rais wa kipindi hicho Thabo Mbeki alijiuzulu baada ya chama cha ANC kuamua kuwa aachie madaraka.

Muungano wa vyama vya wafanyikazi nchini humo COSATU na upinzani wamemtaka rais Zuma kujiuzulu.

Wanasiasa wa upinzani wanasema wanaanda mswada wa kukosa imani na rais Zuma.

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.