Pata taarifa kuu
MALI

Kundi la waasi wa Mali hatimaye limekubali kushiriki mazungumzo ya kitaifa

Kundi la zamani la waasi ambalo lilikuwa limetangaza kususia mazungumzo ya kusaka maridhiano ya kitaifa nchini Mali yaliyoanza juma hili mjini Bamako, limekubali kurejea kwenye mazungumzo hayo baada ya kupewa hakikisho kuhusu kuendelea kwa muda wa mazungumzo kwa muda wa zaidi ya uliokuwa umepangwa.

Wajumbe wanaohudhuria mazungumzo ya kitaifa nchini Mali. Machi 27, 2017.
Wajumbe wanaohudhuria mazungumzo ya kitaifa nchini Mali. Machi 27, 2017. HABIBOU KOUYATE / AFP
Matangazo ya kibiashara

Kundi hilo la vuguvugu la Azawad ambao ni waasi wa zamani wa Tuareg waliokuwa wanapigana kaskazini mwa nchi hiyo kwa pamoja na na upinzani walikuwa wamesusia mazungumzo hayo wakipinga muda wa siku 7 uliokuwa umepangwa kwa mazungumzo hayo kufanyika.

Mazungumzo haya ambayo ni sehemu ya makubaliano ya mkataba uliotiwa saini kati ya Mei na Juni mwaka 2015, unalenga kuwaleta pamoja wanasiasa kwaajili ya amani, umoja na maridhiano nchini humo.

Lakini mwenyekiti wa mazungumzo hayo Baba Akhib Haidara, alisema Jumatatu ya wiki hii kuwa baada ya majadiliano ya kina ya pande zote na kwa kuzingatia mkataba uliotiwa saini, wamekubaliana kwa pamoja kutoweka ukomo wa mazungumzo haya.

Kwa siku ya Jumanne wa wakilishi kutoka kundi la CMA walikuwepo na hii ni kwa mujibu wa muandishi wa habari wa AFP anayehudhuria mkutano huu, ambapo amesema pia msemaji wa makundi ya zamani ya waasi Mohamed Elmaouloud Ramadane nae alikuwepo.

Katika taarifa iliyotolea na mwakilishi wa rais wa Mali kwenye utekelezaji wa mkataba huo wa amani Mahamadou Diagouraga, alitangaza kuwa kundi hilo la waasi lilisema litajiunga kwenye mazungumzo hayo siku ya Jumanne.

Mazungumzo haya pia yanahudhuriwa na wawakilishi kutoka umoja wa Mataifa na umoja wa Ulaya ambao wanafuatilia kwa karibu mchakato wa kufikia maridhiano ya kitaifa kwenye nchi ya Mali.

Nchi ya Mali licha kwa sehemu kubwa kushuhudia utulivu, bado eneo la kaskazini mwa nchi hiyo linakabiliwa na uasi unaofanywa na makundi ya kijihadi ambayo yamekuwa yakitekeleza mashambulizi dhidi ya vikosi vya kigeni vinavyolinda amani nchini humo.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.