Pata taarifa kuu
UN-DRC

UN yataka kufanyike uchunguzi wa matuko ya ukiukaji haki za binadamu DRC

Tume ya haki za binadamu ya umoja wa Mataifa, imetaka kufanyike uchunguzi wa kina kuhusu vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu vilivyofanywa dhidi ya raia wa kawaida kwenye maeneo yenye vurugu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, baada ya kugundulika kwa kaburi la pamoja.

Mkuu wa tume ya haki za binadamu ya umoja wa Mataifa, Zeid Al-Hussein
Mkuu wa tume ya haki za binadamu ya umoja wa Mataifa, Zeid Al-Hussein REUTERS/Denis Balibouse
Matangazo ya kibiashara

Mkuu wa tume hiyo, Zeid Ra'ad Al Hussein, ameipongeza Serikali ya DRC kwa kuchukua hatua za haraka kuchunguza mauaji na matukio mengine makubwa ya unyanyasaji na ukatili uliofanywa kwenye jimbo la Kasai na Lomani, lakini akasema uchunguzi wa umoja wa Mataifa unahitajika pia.

"Napongeza hatua za haraka na mapema zilizochukuliwa na Serikali kuanza mchakato wa kuchunguza na kuwajibika kwa sehemu ya mauaji yanayodaiwa kufanywa na wanajeshi wa Serikali na ofisi yangu iko tayari kutoa ushirikiano," alisema Zeid mkuu wa tume ya umoja wa Mataifa ya haki za binadamu.

Hata hivyo aliendelea kusema kuwa "kupitia ripoti za ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na kugundulika hivi karibuni kwa kaburi la pamoja, nashauri baraza hili liunde tume maalumu kuchunguza tuhuma hizi."

Mwezi Februari mwaka huu, video ya dakika 7 iliyowekwa kwenye mitandao ya kijamii, ambayo ilionekana imerekodiwa kwa simu ya kiganjani, ikionesha mauaji ya watu wasio na silaha wanawake na wanaume waliouawa na wanajeshi  kwenye eneo linalodhaniwa kuwa ni Kasai.

Baadhi ya vijana wakiwa wamechoma matairi kwenye moja ya barabara za Kinshasa
Baadhi ya vijana wakiwa wamechoma matairi kwenye moja ya barabara za Kinshasa https://cdn-images

Nchi ya DRC pia imeshuhudia ikikumbwa na machafuko ya kisiasa baada ya rais Joseph Kabila kukataa kuondoka madarakani mwisho wa muhula wake mwezi Desemba mwaka jana.

Kuendelea kwake kuwepo madarakani kulisababisha maandamano ambayo yalisababisha vifo vya watu 100 mwezi Septemba na mwezi Desemba mwaka jana, alisema Zeid.

"Ofisi yangu itaendelea kufuatilia kwa karibu kuhusu uelekeo wa kisheria wa suala hili na kuchukuliwa hatua kwa wanausalama hawa."

Zeid pia ameelezea kuguswa na kusikitishwa kutokana na kutokuwepo maendeleo yoyote kuhusu kuanza utekelezaji wa mkataba wa Desemba 31 mwaka jana ili kumaliza sintofahamu ya kisiasa.

Mkataba huu utaruhusu rais Kabila kusalia madarakani hadi pale nchi hiyo itakapofanya uchaguzi mkuu mwishoni mwa mwaka huu, lakini unataka kuundwa baraza la Serikali ya mpito.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.