Pata taarifa kuu
CAR-MINUSCA

UN yatekeleza operesheni dhidi ya makundi ya waasi nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati

Operesheni ya vikosi vya umoja wa Mataifa iliyoenda sambamba na mashambilizi ya anga, ilifanikiwa kuwasambaratisha wapiganaji waasi waliokuwa na silaha kwenye mji wa Bambari nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati. 

Askari wa vikosi vya Minusca nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati wakiwa katika moja ya operesheni dhidi ya makundi ya wapiganaji
Askari wa vikosi vya Minusca nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati wakiwa katika moja ya operesheni dhidi ya makundi ya wapiganaji UN Photo/Nektarios Markogiannis
Matangazo ya kibiashara

Zaidi ya wapiganaji 40 kutoka kundi maarufu la Popular Front for the Renaissance of Central African Republic, wakiwa wamejihami na silaha za moto na maroketi walijikusanya kwenye mji huo lakini wakashindwa kutekeleza uasi wao baada ya vikosi vya umoja wa Mataifa kuingilia kati.

Taarifa ya tume ya umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, imesema kuwa, operesheni iliyofanywa na vikosi vyake ilikuwa ni sehemu ya mamlaka waliyopewa kuwalinda raia na kuzuia vita kati ya makundi ya wapiganaji na makundi mengine ya waasi wa UPC.

Msemaji wa MINUSCA, Vladimir Monteiro amesema kuwa, vikosi vyao viliwaonya wapiganaji hao dhidi ya kutekeleza shambulio lolote kwenye mji wa Bambari.

Wapiganaji kutoka kundi la waasi wa FPRC na UPC wengi ni kutoka kundi kuu la waasi wa Seleka ambao ni washirika wa rais wa zamani wa nchi hiyo, Francois Bozize, ambapo makundi haya yamekuwa yakishambuliana na wale wapiganaji kutoka kundi la wakristo wa Anti-Balaka.

Hata hivyo waasi wa Seleka walijikuta wakigawanyika katia makundo haya mawili baada ya kutofautiana kuhusu mapato wanayokusanya kutokana na biashara haramu ya dhahabu na almasi kwenye baadhi ya majimbo.

Kwa mujibu wa shiika la kutetea haki za binadamu duniani Human Rights Watch, linasema kuwa waasi wa UPC waliwaua watu zaidi ya 32 mwezi Desemba mwaka jana baada ya kukabiliana na waasi wa kundi la FPRC.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.