rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Somalia Mohamed Abdullahi Farmajo Al Shabab

Imechapishwa • Imehaririwa

Rais mpya wa Somalia atawazwa Jumatano hii

media
Mohamed Abdullahi Farmajo alichaguliwa kuwa rais wa Somalia, Februari 8, 2017. REUTERS/Feisal Omar

Rais mpya wa Somalia Mohamed Abdullahi Mohamed Farmajo aliyechaguliwa Februari 8, atatawazwa Jumatano hii Februari 22 mjini Mogadishu. Farmajo atakuwa rais wa tisa wa Somalia tangu nchi hiyo kupata uhuru.


Wakati wa kampeni za uchaguzi aliahidi kupambana na rushwa na kuboresha maisha ya Wasomali, hasa huduma za afya nchini humo. Lakini kazi inayomsubiri ni kubwa. Shambulizi la Jumapili mjini Mogadishu lililowaua watu thelathini na tisa linakumbusha kwamba lengo lake kuu ni kurejesha usalama. Farmajo alitoa muda wa miaka miwili ili awe ametokomeza Al-Shabaab, kundi la kigaidi linalondesha vita dhidi ya serikali kwa zaidi ya miaka sita.

Nchini Somalia, suala siyo kufafanua vipaumbele (kila kitu ni kipaumbele) lakini kuchukua maamuzi. Tangu shambulizi la Jumapili, Februari 19 mjini Mogadishu lililoua watu 39, usalama umeendelea kupewa kipaumbele na Rais Farmajo.

Wakati wa mkutano na mabalozi wa Afrika wanachama wa kikosi cha kulinda amani, Amisom, alisema anataka kutokomeza kundi la Al-Shabab katika kwa muda wa miaka miwili. Farmajo hata hivyo alituma wajumbe wake nchini Kenya na Ethiopia kuthibitisha ahadi yake kwa viongozi wa nchi hizi kwamba wanachangia lengo moja, yaani kutokomeza ugaidi.