Pata taarifa kuu
ZIMBABWE-MUGABE-TRUMP

Mugabe asema kufurahishwa na sera za Donald Trump

Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe amesema anamuunga mkono rais wa Marekani Donald Trump na kukubaliana na sera yake kwamba "Marekani yapaswa kuwa tu ni ya Wamarekani".

Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe katika mkutano na maveterani wa ukombozi, Aprili 7 katika Harare.
Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe katika mkutano na maveterani wa ukombozi, Aprili 7 katika Harare. REUTERS/Philimon Bulawayo
Matangazo ya kibiashara

Rais Mugabe amesema hangeweza kufurahi iwapo hillary Clinton angelishinda uchaguzi wa urais nchini Marekani mwaka uliyopita.

Hata hivyo Bw Mugabe, ambaye ni mara ya kwanza anazungumzia utawala wa Bw Trump, amesema alishangazwa sana kuona kiongozi huyo wa chama cha Republican anaibuka mshindi katika uchaguzi wa urais nchini Marekani.

Kwa mujibu wa gazeti la serikali nchini Zimbabwe la Herald, likimnukuu Rais Mugabe limeeleza kuwa rais huyo amemuunga mkono Rais Donald Trump na kusema: “Nilimuunga mono Rais Donald Trump kwa maneno yake ya kuweka mbele uzalendo aliposema Marekani iwe ya Wa Marekani. Na mimi nasema Zimbabwe iwe ya Wazimbabwe.”

Mahojiano kamili ya Bw Mugabe yanatarajiwa kupeperushwa rasmi kesho jioni kwenda sambamba na maadhimisho ya kusherehekea kiongozi huyo kutimiza miaka 93 tangu kuzaliwa kwake.

Itafahamika kwamba Robert Mugabe tayari ameteuliwa na chama tawala cha Zanu-PF kuwa mgombea wake wa urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.