Pata taarifa kuu
SOMALIA-UNICEF-WFP-NJAA

UNICEF na WFP yatoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuisaidia Somalia

Shirika la umoja wa Mataifa linalohusika na watoto UNICEF, pamoja na lile la mpango wa chakula duniani WFP, yameonya kuwa njia pekee ya kuinusuru nchi ya Somalia dhidi ya janga la kibinadamu, ni kwa jumuiya ya kimataifa kutoa msaada wa haraka.

Nchi ya Somalia, hasa , eneo la Putland linakabiliwa na ukame.
Nchi ya Somalia, hasa , eneo la Putland linakabiliwa na ukame. NOAH SEELAM / AFP
Matangazo ya kibiashara

Mashirika hayo yanasema hali hiyo imeenea nchi nzima na inatishia ustawi wa raia zaidi ya milioni 6 wa taifa hilo
ambapo watoto zaidi ya laki 9 na elfu 44 wanasumbuliwa na utapia mlo.

Toka mwanzoni mwa juma hili, maofisa wa UNICEF na wale wa EFP wametembelea maeneo ya Somalia yaliyoathirika zaidi na ukame hasa kwenye jimbo la Puntland, ambako wanasema msaada wa haraka unahitajika.

Somalia inakabiliwa na matatizo mbalimbali ikiwa ni pamoja na vita vya wenyewe kwa wenyewe, hasa kundi la Al Shabab ambalo limekita mizizi nchini humo na ukame ambao unatishia sasa kusababisha janga la njaa nchini Somalia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.