Pata taarifa kuu
DRC-DINI-USALAMA

Polisi yafanya operesheni dhidi ya dhehebu la Bundu dia Kongo mjini Kinshasa

Vikosi vya usalama viliendesha operesheni dhidi ya malengo ya dhehebu la Bundu dia Kongo mjini Kinshasa. Inaarifiwa kuwa watu kadhaa waliuawa katika operesheni hiyo na wengine kadhaa walijeruhiwa kwa risasi.

Muanda Nsemi, Kiongozi wa kiroho wa dhehebu la Bundu dia Kongo, wakati wa Misa (BDMCANADA, Julai 2016).
Muanda Nsemi, Kiongozi wa kiroho wa dhehebu la Bundu dia Kongo, wakati wa Misa (BDMCANADA, Julai 2016). youtube.com
Matangazo ya kibiashara

Kiongozi wa kiroho wa dhehebu hili ametishia utawala uliopo madarakani katika video iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii. Muanda Nsemi amesema ana mashaka na uraia wa Rais Joseph Kabila na amewaomba watu wasio kuwa wazaliwa wa Kongo ya kati kuondoka katika jimbo hilo.

Milio ya kwanza ya risasi ilisikika wilayani Ngiri-Ngiri. Waumini wa dhehebu hilo la Bundu dia Kongo, ndio walianza kufyatua risasi, chanzo kilio karibu na operesheni hiyo kimeeleza. Kwa mujibu wa chanzo hicho, polisi walikua walikuja kuwaondoa watu thelathini ambao walikuwa wamejificha katika nyumba moja, wakisubiri kufanya machafuko katika mji mkuu.

Madai haya yamekanushwa na katibu mkuu wa dhehebu la Bundu dia Kongo (BDK) ambaye amesema kuwa lilikua shambulizi dhidi ya nyumba ya pili ya Muanda Nsemi, kiongozi wa kiroho wa dhehebu hiloi. Kwa mujibu wa Bw Futila ambaye pia amebainisha kuwa shambulio hili lilianyika wakati wa waumini wa dhehebu hilo walikuwa katika sala.

Makabiliano hayo pia yalishuhudiwa katika kata ya Joli Park katika mji wa Ngaliema, ambapo kunapatikana makaazi ya kiongozi wa kiroho wa dhehebu la Bundu dia Kongo. Mashahidi wanasema katika nyumba hiyo kulikuepo na wanawake, watoto na wazee waliokusanyika katika sala. katika siku za hivi karibuni, Muanda Nsemi amekua akijitokeza kwa hotuba mbalimbali wambazo serikali imezitaja kuwa ni za "kibaguzi" na zenye "matusi kwa mkuu wa nchi."

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.