Pata taarifa kuu
DRC-DINI-USALAMA

Makabiliano kati ya wafuasi wa Bundu dia Kongo na polisi mjini Kinshasa

Makabiliano hayo yalitokea Jumapili hii asubuhi katika mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Kinshasa wakati wa operesheni ya polisi dhidi ya nyumba ya kiongozi wa vuguvugu la kisiasa lililopigwa marufuku la Bundu dia Kongo, linaloshtumiwa na serikali kuchochea vurugu Magharibi mwa nchi.

Moja ya makaazi ya kiongozi wa dhehebu la Bundu dia Kongo, Muanda Nsemi, wilayani Ngaliema katika kata ya Joli Parc mjini Kinshasa. Makaazi haya yamezingirwa na polisi , Februari 14, 2017.
Moja ya makaazi ya kiongozi wa dhehebu la Bundu dia Kongo, Muanda Nsemi, wilayani Ngaliema katika kata ya Joli Parc mjini Kinshasa. Makaazi haya yamezingirwa na polisi , Februari 14, 2017. RFI/Sonia Rolley
Matangazo ya kibiashara

Katika video iliyorushwa hivi karibuni kwenye intaneti, kiongozi vuguvugu hilo alitoa wito wa kukabiliana dhidi ya serikali ya Rais Kabila.

Jumanne mchana, makabiliano yalikua bado yakiendelea kati ya wafuasi wa vuguvugu hilo na polisi.

Hali ilikua bado tete Jumanne wiki hii mchana kwa sababu ilitangazwa kutokea kwa shambulizi la polisi. Hivyo ndivyo walivyofikiri wafuasi wa vuguvugu hilo ambao waliweka vizuizi karibu na nyumba ya kiongozi wa dhehebu la Bundu dia Kongo. Magari tano, angalau, yalichomwa moto.

Wafuasi wengi walikua ndani ya nyumba hiyo lakini haijajulikana kama kiongozi wa vuguvugu hilo, Muanda Nsemi, yupo ndani ya makaazi yake au la. Waumini ambao wako ndani ya makaazi ya kiongozi huyo wakifanya maombi hawataki kusema iwapo wako naye ndani ya nyumba hiyo.

Inaarifiwa kuwa ndani ya nyumba hiyo kuna watu waliojeruhiwa na wengine waliouawa. Nje kuna kundi la watu ambao waliweka vizuizi, huku wengine wakipiga doria nje ya makaazi ya kiongozi uyo.

Hayo yakijiri miili kadhaa ya watu waliokufa imepatikana kwenye eneo la Kya Ala katika ufalme wa Bwito mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, wakati huu jeshi la serikali (FARDC) likiendelea kuwasaka waasi wanaojihusisha na vitendo vya utekaji nyara kwenye eneo la mashariki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.