Pata taarifa kuu
UGANDA-DRC

ICGLR kuzindua kituo cha Inteljensia nchini Uganda

Mataifa ya Ukanda wa Maziwa Makuu ICGLR mwisho wa mwezi huu yanatarajiwa kuzindua kituo maalum cha Kiinteljensia Wilayani Kasese nchini Uganda, kuchunguza hali ya usalama Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Waasi wa FDLR Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Waasi wa FDLR Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo AFP PHOTO / Roberto SCHMIDT
Matangazo ya kibiashara

Kituo hicho kitaundwa na maafisa 12 kutoka mataifa yote ya Ukanda wa Maziwa Makuu, watakaofanya kazi ya kukusanya taarifa muhimu za kiusalama kusaidia kupambana na makundi ya waasi Mashariki mwa DRC hasa kundi la ADF NALU.

Kundi la ADF ambalo limetuhumiwa kutekeleza mauaji ya mamia ya watu Mashariki mwa DRC, limekuwa likituhumiwa kuwasajili wapiganaji kutoka kundi la Al Shabaab nchini Somalia na Boko Haram kutoka Nigeria.

Mkurugenzi Mkuu wa  ICGLR Zachary Muburi-Muita, ameliambia Gazeti la The East African amesema kituo hiki kitasaidia kupambana na makundi haya ya waasi ambayo yanaelezwa yamekuwa yakifanikiwa kwa sababu hakuna taarifa za Kiiteljensia kupambana na makundi hayo.

Licha ya kufanikiwa kuwaondoa waasi wa M 23, wanajeshi wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania, Malawi na Afrika Kusini wameonekana kushindwa kukabiliana na makundi kama ADF NALU, FDLR, Mai Mai na makundi mengine ya waasi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.