Pata taarifa kuu
MSUMBIJI

Msumbiji: Renamo yatangaza kusitisha mapigano kwa miezi miwili zaidi

Waasi nchini Msumbiji wametangaza nyongeza ya muda wa miezi miwili kusitisha mapigano na Serikali, tangazo linalotoa matumaini ya kupatikana kwa amani baada ya kuzuka kwa mapigano mwaka jana ambapo watu kadhaa walikufa. 

Afonso Dhlakama, kiongozi wa kundi la Renamo
Afonso Dhlakama, kiongozi wa kundi la Renamo Cristiana Soares
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Msumbiji amesema kuwa, tangazo lililotolewa na rais wa kundi la Renamo ambalo pia ni chama cha upinzani, Afonso Dhlakama, limeonesha imani iliyoko baina ya pande hizo mbili katika kutafuta muafaka.

Mgogoro uliozuka mwaka jana kati ya Serikali inayoongozwa na chama cha Frelimo na waasi wa Renamo, umesababisha kufufuka kwa hisia kali na hofu nchini humo, taifa ambalo lilishuhudia vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyomalizika miaka 20 iliyopita.

Hata hivyo kiongozi wa Renamo, Dhlakama, amesema kuna matukio kadhaa yaliyojitokeza lakini akasema muda wa siku saba wa kusitisha mapigano umedumu vizuri na hivyo naongeza muda wa siku 60 zaidi hadi Machi 4.

"Usitishaji huu wa mapigano unalenga kujenga hali ya mazingira mazuri kuendelea mbele na mazungumzo mjini Maputo, mazungumzo yatakayoleta maridhiano kwa pande zote.

Dhlakama, ambaye anaishi mafichoni kwenye milima ya Gorongosa katikati mwa nchi na kuongeza kuwa vikosi vya Renamo havitashambulia wanajeshi wa Serikali wala ngome zao.

Mwaka jana mapigano yalishuhudiwa na watu zaidi ya elfu 15 wamelazimika kukimbia maeneo yanayoshikiliwa na vikosi vya Serikali na kukimbilia kwenye nchi za Malawi na Zimbabwe.

Tangazo hili limekuja baada ya juhudi za kina kufanyika ili kuruhusu kufanyika kwa mchakato wa amani ambao ulivunjika mwaka jana baada ya pande hizo mbili kutofautiana pakubwa ikiwemo kuuawa kwa mpatanishi wa Renamo.

Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi, amesema kuwa tangazo la kusitisha mapigano ni chanya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.